Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,Amina Makilagi amefungua Mafunzo ya kuandika habari mwendelezo za Sensa kwa Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa, ambayo yameandaliwa na Chama cha Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Nchini Tanzania ( OJADACT )
Mwenyekiti wa Chama cha Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Tanzania ( OJADACT ) Edwin Soko,amewataka waandishi wa habari kuandika habari za Sensa kwa kufuata misingi ya uandishi wa habari pamoja na weredi ili ziweze kuleta tija kwa jamii
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Tanzania ( OJADACT ) Edwin Soko,ametoa wito wa kutopotosha takwimu za Sensa pamoja na kuweka taarifa sahihi zilizotoka kwenye eneo lililohesabiwa ikiwemo mitaa na vijiji.
Awali akifungua semina hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Amina Makilagi amekipongeza Chama cha Kupiga Vita Dawa za Kulevya Tanzania ( OJADACT ) kwakuwa cha kwanza Tanzania kutoa Semina ya Uandishi wa habari za Sensa Kanda ya Ziwa.
0 Comments