Header Ads Widget

MTANZANIA MFUPA ASHINDA PAMBANO LAKE UINGEREZA

 


Kassim Selemmani Mbundwike aka Mfupa wa Sokwe leo ameshinda kwa kishindo cha RSC ama Refa Kusimamisha pambano katika 

ya tatu ya pambano lake la Robo fainali dhidi ya Marion Faustino AH Tong kutoka nchi ya Samoa katika bout no. 162 katika uzani wa Light middleweight 67kg - 71kg


Na tayari Mfupa huo wa Sokwe umejihakikishia kupata medali ambayo itakua ya pili kwa upande wa Ngumi, na ya tatu kwa Team Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza.


Mbundwike anajiunga na askari mwenzie wa JWTZ mwenye cheo kama yeye cha 'Private', Yusufu Changalawe, katika mpambano wa nusu fainali siku ya Jumamosi na kama wakishinda wataingia fainali Jumapili kugombea

Medali za dhahabu ama Fedha. 


Hapo walipo wote tayari wana medali za shaba


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI