Header Ads Widget

MPAMBALYOTO ACHAGULIWA TENA MAKAMU MWENYEKITI LUDEWA

 


Na Gabriel Kilamlya , MatukioDaimaAPP Njombe

BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Ludewa limemchagua Kwa kipindi cha   pili diwani wa kata ya Mawengi Bwana Leodgar Mpambalyoto amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.


Baada ya kupigwa kwa kura hizo katika mkutano wa baraza la madiwani  mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias ametangaza matokeo na kwamba bwana Mpambalyoto amepata kura 29 kati ya 31 zilipigwa ikiwa moja imeharibika na moja imekuwa ya hapana.


Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa na madiwani hao makamu mwenyekiti Mpambalyoto amewashukuru madiwani wote waliompigia kura kwa kumuamini huku akisema kura moja ya hapana inamfundisha kuwa kuna baadhi ya mambo hakuyafanyia kazi vilivyo jambo linalomfanya kwenda kufanya tathmini.



Amesema ataendelea kushirikiana na kila mmoja katika kutekeleza shughuli za maendeleo pamoja na kumsaidia mwenyekiti katika kusukumu gurudumu la maendeleo.


Katika uchaguzi huo pia zimechaguliwa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri zitakazohudumu katika kipindi cha mwaka mmoja.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI