MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amesema kuwa zoezi la Sensa ni muhimu kwa kila mwananchi kwani linaleta maendeleo.
Zuena ametoa kauli hiyo jana alifokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Makuyuni Jimbo la Vunjo wilayani Moshi ambapo alisema kuwa Sensa ndiyo inayopanga maendeleo kulingana na idadi ya wananchi wa eneo husika.
Alisema kuwa, Agosti 23 mwaka huu ni tarehe ambayo kila mwananchi anawajibu wa kuamkia anapoishi ili kuhesabiwa na kusaidia maendeleo katika eneo husika.
"Zoezi la Sensa halifungamani na itikadi yoyote ya chama hivyo niwaombe wananchi wote bila kujali itikadi zetu tushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ili tujiletee maendeleo yetu" alisema Mbunge Zuena.
Alisema mbali na maendeleo zoezi hilo la Sensa pia linaisaidia Serikali kutambua idadi ya wananchi wake na kuwataka kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu pamoja na wazee kwani nao wanahaki ya kuhesabiwa.
Mwisho...
0 Comments