Na Gabriel Kilamlya ,Matukio Daima App Njombe
Halmshauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imeripotiwa kufikia zaidi ya asilimia 90 katika zoezi la Sensa ya watu na makazi hadi usiku wa Agosti 25 mwaka huu.
Kwa mujibu mwenyekiti wa sensa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo amesema kati ya watu zaidi ya elfu 35 wanaopaswa kuhesabiwa hadi Sasa wameshahesabiwa zaidi ya watu elfu 32 ambapo Kesho wanatarajia kumaliza kazi hiyo.
Tsere ametoa ripoti hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye anakagua utekelezaji wa zoezi la sensa wilayani Ludewa.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amesema licha ya mafanikio hayo makubwa lakini kumekuwapo kwa changamoto mbalimbali hususani mawasiliano magumu mwambao mwa ziwa nyasa pamoja na ukosefu wa fedha za mafuta ya boti.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amepongeza hatua iliyofikiwa katika Wilaya ya Ludewa na kwamba wanapaswa kukamilisha kazi hiyo kwa maslahi mapana ya taifa.
0 Comments