Header Ads Widget

WAZIRI DKT. GWAJIMA AKOSHWA MAONESHO YA 46 SABASABA

 


Na WAMJW- DSM


Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameelezea kufurahishwa kwake na Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam na kusema atatumia fursa alizozibaini katika maeneo tofauti aliyotembelea wakati wa ziara yake ziwe  fursa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii.  


"Nimepita kwenye taasisi za Benki, kilimo,  SIDO, Ustawi na Maendeleo ya Jamii, kama Wizara tunachotaka sasa ni kuunganisha ngivu baina ya Wizara za Kisekta" amesema Mhe. Gwajima.



Dkt. Gwajima amesema amebaini zipo fursa nyingi lakini zimekuwa zikikosa msukumo wa Kisera hivyo akaahidi kwa kutumia Mifumo ya Serikali watafanikisha  suala hilo.



Aidha, Waziri Gwajima pia amekutana na vijana wazalendo wanaoendesha Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) kwa lengo la kupinga vitendo vya ukatili Banda la Wizara na kuwapongeza wazalendo hao kwa kuisaidia Jamii kupambana na vitendo hivyo. 



Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwenyekiti wa SMAUJATA Sospeter Bulugu, amesema wao kama Vijana wa Kitanzania watatumia kila fursa wanayoina kujifunza na kuhakikisha wanaikomboa jamii ya Kitanzania na Ukatili.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI