Header Ads Widget

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSIMAMIA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO

  

NA HADIJA OMARY , MATUKIODAIMAAPP,LINDI

WAZAZI na Walezi Mkoani Lindi wametakiwa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia swala la malezi na makuzi ya Watoto wao kwa mustakabali wa Taifa Endelevu


Wito huo umetolewa na katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi B Rehema Madenge wakati wa uzinduzi wa Programu jumuishi ya kitaifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT MMMAM) iliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya maonysho ya Nane Nane Ngongo Manispaa ya Lindi.


Madenge alisema ili kufikia Taifa Imara wazazi na walezi hawana budi kushirikiana kwa pamoja katika malezi ya Watoto kuanzia katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla



“Kwetu sisi huu sio uzinduzi kwa sababu uzinduzi ulishafanyika kitaifa kikubwa ni kuamasisha uelewa wa swala zima la malezi na makuzi ya Watoto kuanzia Mwaka  0 - 8 katika Mkoa wetu wa Lindi ” alieleza Madenge 


Aidha Bi. Madenge aliongeza kuwa Maswala ya malezi na makuzi ya mtoto ni swala mtambuka halihusu mtu mmoja wala watu wawili bali linatuhusu watu wote kwa umoja wao katika jamii


” Ndio maana sote tupo hapa leo kwamba tujitahidi kadri inavyowezekana tuhakikishe kwamba tunasimamia swala zima la malezi na makuzi ya watoto wetu maana siku izi ipo tabu ya Watoto kutokukanywa na mtu ambae sio mzazi wake kwa maana kwamba mtoto huyu akijaribu kumkanya mtu mwingine wazazi wanakuja juu, kumbe tunatakiwa tuambizane na sote katika jamii tunatakiwa kufahamu kama vile tulivyokuwa tunalelewa sisi kwamba yeyote aliekuzidi umri anao wajibu wa kukufundisha”. Alieleza 


Kwa upande wake Shabani Muhari Ofisa  kutoka ofisi ya Rais Tamisemi Idara ya Afya ustawi wa Jamii na Lishe alisema kuwa program hiyo jumuishi ya kitaifa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto ijulikanayo kama (MMMAM) inatekelezwa kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 inalenga la kuongeza kasi ya mafanikio yanayopatikana katika huduma kwa kuboresha ushirikiano wa sekta katika utoaji wa huduma za malezi jumuishi kwa Watoto.


Alisema program hiyo pia inagusa maeneo matano ya mfumo wa malezi jumuishi ambayo ni Afya Bora, Lishe, malezi yenye muitikio , fursa za ujifunzaji pamoja na ulinzi na usalama  ambayo yataongeza kasi ya mafanikio yanayopatikana katika malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kwa kuimarisha ushirikiano wa wadau mbali mbali wa Sekta katika utoaji wa huduma jumuishi kwa Watoto.


“Program jumuishi ya MMMAM inalengo la kushughulikia mahitaji mahususi yaliyotambuliwa baada ya kufanya uchambuzi wa hali halisi ya huduma za malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kwa Watoto wenye umri wa Miaka 0-8 hapa Nchini Tanzania'’.

Kwa upande wake Bwana Christopha pater ofisa kutoka Mtandao wa Malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto Tanzania (TECDEN) alisema kuwa swala la malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto hasa wenye umri wa miaka 0-8 unamchango mkubwa na chanya katika kutengeneza kizazi au Watoto ni muhimu katika Taifa la baadae.

Alisema ili kufikia malengo yanayotarajiwa kwenye Programu hiyo kila  mdau alieguswa kwenye Programu anaowajibu kutekeleza ipasavyo. 

“sisi kama TECDEN tunashirikiana na Wizara za kisekta na wadau tofauti katika kuhakikisha katika hii program jumuishi ya Malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya Watoto kwa kuwekeza Rasilimali Fedha na watu ili program iweze kuleta matokeo chanya”

Nae ofisa ustawi Mkoa wa Lindi Stela Kihombo amesema kuwa baada ya uzinduzi huo wao kama watekelezaji wakubwa wa Programu hiyo wamejipanga kutekeleza program hiyo kama ilivyopangwa .

"Hii ni kazi ambayo tulikuwa tunaifanya  karibia kila siku lakini kwa kuwa imekuja hii Progam ikiwa maboresho zaidi kazi yetu sisi ni kuyachukua hayo maboresho na kuyafanyia kazi kwa lengo la kuwasaidia au kuokoa kizazi chetu cha Watoto wetu wa huku Lindi lakini mwisho wa siku tuweze kupata watoto wa Taifa Imara la baadae" alisema Kihombo 

Kwa upande wake zuhura Abdaha kutoka chama cha watu wenye ulemavu pamoja na kuishukuru Serikali ya Mkoa huo kwa kushirikisha kundi hilo la watu wenye ulemavu pia alisema kuwa endapo program hiyo itatekelezwa kama inavyosemwa italeta matokeo chanya kwa Watoto na jamii kwa ujumla




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI