Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Ili kuhakikisha sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika August 23 mwaka huu inafanikiwa kwa asilimia 100 wilayani Njombe ,Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Gwakisa Kasongwa amelazimika kupita kijiji kwa kijiji katika halmashauri 3 zinazounda wilaya Hiyo na kutoa elimu.
Mbali na timu ya ulinzi na usalama kujiwekea mkakati huo ili wananchi wote wapate haki ya kuhesabiwa lakini Mkuu wa wilaya ameagiza kila mkutano wa kiserikali kuanzia ngazi ya chini kabisa kuifanya agenda ya sensa kupewa kipaumbele.
Akiwa katika zoezi la kutoa elimu katika vijiji vya Usetule,Kifumbe,Ibatu na Mahongole timu ya ulinzi na usalama ambayo imeongozana na watalaamu kutoka idara tofauti za kiserikali Mratibu wa Sensa Halmashauri ya mji wa Makambako Igbert Kindimba amesema ili kuhakikisha kila mtu anapata fursa na haki ya kuhesabiwa serikali wilayani humo imeweka utaratibu wa namna ya kuhesabu katika vituo vya reli inayopita katika vijiji tofauti vya mji wa Makambako huku Nyumba za kulala wageni nazo zikiwekewa mpango madhubuti.
Awali mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema wananchi wanapaswa kutambua faida za kujiandikisha na kuhesabiwa kwasababu kupitia zoezi hilo serikali inaweka mipango ya maendeleo na kutoa huduma za kijamii kulingana na mahitaji.
Mara baada ya kutoa elimu hiyo kwa wananchi ndipo nao akiwemo Modestus Augustino wakatoa maoni yao juu ya zoezi hilo
Katika ziara hiyo pia mkuu wa wilaya anatoa elimu ya UVICO 19 ili wananchi waweze kuendelea kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga na gonjwa hilo hatari.
0 Comments