Header Ads Widget

VIONGOZI WAPYA CCM WATAKAO CHAGULIWA WILAYANI MBINGA WANATAKIWA KUISIMAMIA SERIKALI KIKAMILIFU_ SIAYI

 


Na Amon Mtega _Mbinga.


VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma watakaopata nafasi ya kuchaguliwa na wanachama wanatakiwa kuisimamia Serikali kikamilifu kwenye utekelezaji wa ilani ya Chama ili Wananchi waendelee kukichagua chama hicho kuongoza Dola.


Wito huo umetolewa na katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Jacob Siayi wakati akifungua kikao cha Baraza maalumu cha Jumuiya ya wanawake UWT Wilayani humo ambalo lilikuwa rasmi kwaajili ya kujadili mapendekezo ya majina ya kuwania uongozi wa Jumuiya hiyo kutoka kwenye kata za Wilaya hiyo.


 Siayi akifungua mkutano huo pamoja na kupokea taarifa za utendaji kazi kutoka kwa madiwani wa vitimaalumu waliyotokana na chama hicho  amesema kuwa CCM pamoja na Jumuiya zake wakati wa uchaguzi ndiyo wanaopita kuomba ridhaa kwa Wananchi ya kushika dola kwa kuinadi ilani hivyo kuna kila sababu ya kila kiongozi wa Chama hicho atakayepewa dhamani ya kuongoza kwenda kuisimamia Serikali kikamilifu.



 "Naomba tuwe wakweli kipindi cha uchaguzi hatulali kila mwanaccm anakuwa na kazi ya kuwaomba Wananchi wakipatie Chama cha Mapinduzi  ridhaa ya kushika dola hivyo Viongozi watakaochaguliwa wailinde heshima hiyo kwa kuisimamia Serikali kikamilifu "amesema katibu Jacob Siayi.


Hata hivyo katibu huyo amewataka wakangaze kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuhamasisha suala la sensa mwaka huu.


Katika hatua nyingine katibu Siayi amewataka wanawake kuacha kuwaza muda wote wa hamsini kwa hamsini wakati huko walishapita wanauwezo wa kufanya makubwa zaidi.



Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya wanawake UWT Helmina Makiya amesema kuwa Jumuiya hiyo ipo imara na kuwa itawapata Viongozi Wazuri ambao wanatambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

    

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS