Header Ads Widget

TOS WABEBESHWA MZIGO WA KUHAMASISHA MADAKTARI KUJIUNGA NA PROGRAMU YA SARATANI

 



Teddy Kilanga_Arusha.



Chama cha madaktari bingwa wa maradhi ya Saratani(TOS) kimetakiwa kuhamasisha madaktari waliomaliza masomo na wanaofanya kazi kujiunga katika kusomea programu ya Saratani(oncology) ili kuweza kuondokana upungufu wa madaktari bingwa wa Saratani ambao mpaka sasa wapo 38 nchi nzima.




Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa taasisi ya Saratani Ocean road  Dkt Julius Mwaisilage  wakati akisoma hotuba ya waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika ufunguzi kongamano la kwanza la kimataifa la Saratani lilijumisha wataalamu na wadau ambapo alisema kuwa kutokana na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa wa Saratani daktari mmoja kwa mwaka anahudumia wagonjwa 1200. 




Dkt Mwaisilage amesema kama chama wana malengo yao lakini kikubwa wahamasishe wataalamu waweze kusomea kwani serikali inatoa ufadhili kila mwaka kwa kupeleka fedha chuo kikuu cha Afya na sayansi shirikishi Muhimbili(MUHAS) hivyo wawahamasishe ili kupunguza upungufu huo.




Aidha amesema kuwa kulingana na takwimu wanazoziona katika hosipitali kwa mwaka wanawaona wagonjwa 14600 sawa na asilimia 33 ambapo idadi hiyo ni ndogo kwani Tanzania ina zaidi ya wagonjwa elfu 42 wa Saratani.





Kwa upande wake Rais wa TOS,Dk.Jerry Ndumbaro amesema lengo la kongamano hilo la kimataifa ni kubadilishana uzoefu wa kisayansi katika kuboresha huduma kwenye eneo la saratani ikiwa idadi ya wagonjwa kwa sasa wanaongezeka hasa maeneo ya vijijini.




"Mpango wetu ni kuwafikia watumishi wa afya nchi nzima  walioko katika ngazi ya mkoa na wilaya  katika kuwawezesha wataalamu kugundua  ugonjwa huo mapema ili wagonjwa waweze kutibiwa,"amesema Dk.Ndumbaro.




Pia amesema kupitia chama hicho wanampango mkakati wa kufanya  huduma za upimaji na ugunduzi wa mapema  wa saratani katika jamii ambapo watapita kila mkoa kuhakikisha huduma hiyo inawafikiwa wananchi wa ngazi zote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI