Header Ads Widget

ERASTO MPETE ACHAGULIWA KUWA M/KITI MPYA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE

 



Na Gabriel Kilamlya NJOMBE


Kwa kauli moja madiwani wa Halmashauri ya mji wa Njombe wamepiga kura ya ndiyo ya kumchagua Erasto Mpete kuwa mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo baada ya aliyekuwepo Romanus Mayemba kufariki mwaka mmoja uliopita.


Erasto ambaye ni Diwani wa kata ya Utalingolo ameshinda nafasi hiyo baada ya kuhudumu kwa takribani mwaka mmoja kama Makamu mwenyekiti na Chama cha mapinduzi CCM Taifa Kilirejesha jina moja kati ya majina sita ya madiwani waliochukua fomu kutaka kugombea nafasi hiyo. 


Akitangaza matokeo hayo kaimu katibu tawala wilaya ya Njombe Bwana Melchow Kisinini amesema bwana Mpete amepata kura zote 15 zilizopigwa na madiwani hao.


Baada ya matokeo hayo Mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo Ndugu Erasto Mpete anasema yupo tayari kushirikiana na kila mmoja katika kuiletea maendeleo Halmashauri.



Kissa Kasongwa ni mkuu wa Wilaya ya Njombe ambaye mbali na kupongeza ushindi huo lakini anamtaka Mpete kwenda kusimamia kikamilifu miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo huku Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary akitaka kuendelezwa vyema kwa jitihada za ukusanya mapato.


Sure Mwasanguti ni katibu wa Chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe ambaye anatoa onyo kali kwa watakoendekeza makundi baada ya kumpata Mwenyekiti huyo.



Baada ya kumpata mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya mji wa Njombe kilichosalia ni kusubiri mchakato wa kumpata Makamu mwenyekiti pamoja na uchaguzi mdogo wa diwani wa kata ya Njombe mjini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI