Imeelezwa kuwa kundi la watu wenye ulemavu ,mazingira wanayoishi yamekuwa yakiharibiwa na wao kuwa waathirika wakubwa hivyo mradi wa youth project la shirika la word vision wameweka kipaumbele katika makundi hayo ili kiwatengenezea mazingira mazuri ambayo yatawafanya waishi Kama wengine.
Hayo yamesemwa Deogratius martin. meneja wa mradi wa yuouth project kutoka katika shirika la word vision Tanzania wakati alipokuwa katika mashindano ya westi Kili Forest challenge yaliyofanyika wilayani siha Kilimanjaro.
"sisi kama Shirika tumeamua pia kujikita katika maswala ya vijana katika hivyo basi tunafanya shughili za utunzaji wa mazingira, kwa kuanzisha bustani za upandaji miti ,na miradi ya ufugaji nyuki kwa lengo zima la kufanya wao kuwa sehemu ya Jamii ya watanzania"Alisema degratiu.
Amesema kuwa Kama shirika wamekuwa Ni sehemu ya mafanikio kwa jamii na wameshiriki katika mashindano hayo Kama vijana kuonesha kuwa wanahamasisha utunzaji wa mazingira na kuwasidia watu kwenye suala zima la utalii wa ndani .
Aidha ameendelea kusema Kama mradi wa word vision wanaendelea kuwaeleza wadau kuwa Nchi ya Tanzania imejaliwa rasilimali nyingi ,kwani kuna mbuga za wanyama ,misitu ya asili na ya kukatwa tuendelee kuhamasisha utalii wa ndani kwani tukifanikiwa hivyo itakuwa Ni jambo jema
Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa mabadiliko ya Tabia ya Hali ya Nchi hayamgusi Mtu baki kwa sababu ya mazingira yanapoharibika yanapoharibika yanawaathiri watu wote pamoja na kuathiri hali ya hewa .
0 Comments