Header Ads Widget

WANANCHI KIBITI WAHIMIZWA KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA




WANANCHI wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani wametakiwa kushiriki zoezi la sensa ili serikali iweze kutenga bajeti ya maendeleo kwa kujua idadi ya watu wake.


Hayo yalisemwa Wilayani Kibiti na Meneja wa Benki ya NMB tawi Kibiti Raphael Mbuya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi fulana kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo zenye ujumbe wa Sensa.


Mbuya alisema kuwa  sensa ni suala la kitaifa ikiwa na lengo la kujua idadi ili kuweze kupata maendeleo baada ya kujuaa idadi ya wananchi.


"Sensa ni jambo muhimu kwa kujua idadi ya watu wako wangapi kwani ukishajua idadi ya watu ni rahisi kupanga bajeti ya shughuli za maendeleo,"alisema Mbuya.


Alisema hata kwa benki sensa itasaidia kujua idadi ya watu waliowafikis na wale ambao bado hawajafikiwa na huduma za kifedha ili wapelekewe huduma hiyo muhimu.


"Sensa ni muhimu hata sisi itatusaidia kujua eneo gani hatujafika kujua wako watu wangapi ili tuweze kupanga bajeti zetu za namna ya kuwahudumia wananchi,"alisema Mbuya.


Aidha alisema kuwa waliamua kutoa fulana hizo kwa Madiwani kwani ni wadau wao wakubwa na wao wataweza kufikisha haraka ujumbe wa Sensa ikizingatiwa wao ni wawakilishi wa wananchi. 


Akizungumzia kuhusu huduma za kifedha alisema kuwa wanatoa Mikopo ya aina tofauti na kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii.


"Tunatoa Mikopo kwa ajili ya wakulima, wafugaji na wastaafu na mtu mmoja mmoja ili waweze kuendeleza shughuli zao za kiuchumi kwa lengo la kujiongezea kipato,"alisema Mbuya.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI