Wizara ya utalii Wizara ya maliaasili.na utalii kupitia Bodi ya utalii Tanzania-TTB- imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya Mpira wa kikapu -TBF-ya vijana chini ya miaka 18 inayotarajia kushiriki mashindano ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 18 yatakayofanyika nchini Uganda ikiwa ni moja wapo ya mkakati wa kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa Mpira wa kikapu katika ofisi za bodi ya utalii jijini Dar es salaam kwa niaba ya katibu mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii kaimu mkurugenzi mkuu bodi ya utalii Tanzania Felix John amesema vifaa hivyo vitasaidia kuendeleza mkakati wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini
FELIX John ambaye ni kaimu mkurugenzi mkuu -TTB Alisema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa kuendelea michezo na fursa ya kutangaza utalii ambapo ametaja vifaa vilivyotolewa ni jezi 24 ikiwa ni pea mbili kwa kila timu wa kike na wa kiume,traki suti 35, na soksi 48.ambapo jumla ya gharama zote ni shilingi 6,766,120,
Kwa Sasa tunaendelea na mkakati wa kutanga vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini hivyo mashindano haya ni chachu ya kutangaza utalii hapa nchini na vijana hawa tunaamini kupitia jezi ambazo tumeweka maandishi ya kuhamasisha utalii wetu ,
Alisema John"
Rais wa shirikishi wa mpira wa kikapu hapa nchini Michael Kadebe amesema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza Ari katika mashindano hayo na kuwaahidi watanzania katika mashindano kuleta ushindi nyumbani na kutangaza vivutio ili kuongeza uchumi kupitia fursa ya michezo.
Naishukuru serikali kupitia Wizara ya utalii kutoa vifaa hivyo ambavyo vitatumika katika mashindano hayo.yanayotarajia kuanza tarehe 13-18tunatarajia kutumia fursa hii kutangaza nchi,Alisema kabete"
Timu yetu imeondoka na msafara wa vijana 12 wa kike ,12 wa kiume viongozi pamoja ,kocha na daktari tunategema mashindano hayo tunahiji kendeleza kujenga jamii kuanzia utotoni wanatambau vivutio vilivyopo na kujua kiwa michezo ni fursa muhimu katika jamii,alisema Kadebe"
Zaidi ya shilingi milioni sita ifaa vilivyotolewa ni jezi 24,kwa vijana wa kike na 24 kwa vijana wa kiume traksuti 35,soksi pamoja na Mpira,na mashindano hayo yanafanyika nchini Uganda kuanzia tarehe 13- 18 mwezi wa sita.






0 Comments