Na Chausiku Said MatukioDaimaAPP Mwanza
Vijana wametakiwa kutumia utalamu na ujuzi walioupata vyuoni katika kuleta maendeleo kwenye jamii na kuijenga nchi bila kuwa na hofu.
Hayo yamebainishwa na Katibu uchumi na fedha Taifa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu CCM Dr Frank Hawasi katika mahafari ya kumi (10) ya wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu makada wa Chama cha mapinduzi, mahafali hayo yaliyo jumuisha wahitimu mia tano (500).
Dr, Hawasi ameeleza kuwa vijana wanapaswa kutumia elimu waliyoipata kuletaushirkiano na kuweza kuyafikia malengo, kuwa na ushirikiano pamoja na kutekeleza ahadi ya chama na wanachama kwa ujumla.
"Ni kosa kupata utalamu alafu ukaa nao bila kuipeleka kwa jamii, Mwalimu Nyerere alisema Taifa kusomesha watu wake ni kwa ajili ya Taifa lenyewe" Alisema Dr, Hawasi
Amefafanua kuwa Taifa ambalo hawapendi kujifinza watabaki nyuma katika kuleta maendeleo kwa Taifa na kushiriki katika kiluchochea uchumi na kuwa na moyo wa uzalendo.
"Atakaye heshimisha Taifa ni nyini wenyewe vijana wa senet hakuna atakaye toka nje ya nchi kuja kusemea kutusemea" Alisema Dr, Hawasi.
Kwa upande wako mkuu wa wilaya ya Nyamagana ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Engineer Robert Gabriel amesema wahitimu kuacha anwani ambazo zitawasaidia kupatikana na kuwapatia ajira pamoja na kufanya kazi kwa bidii katika kuliletea maendeleo taifa.
"Nyie ni zao la CCM hakikisheni mnaacha anwani za makazi ya kudumu ili pale mtakapohitajika tuwapate kwa urahisi "alisema Makilagi
Katibu Senet idara ya vyuo na vyuo vikuu Mkoa wa Mwanza ameeleza kuwa Mkoani humo wamefanikiwa kuongeza wanachama kutoka 1400 hadi kufikia 2000 ingawa idadi hiyo huongezeka na kupungua kutokana na udahili wa wahitimu wa wanachuo vyuoni.
Ameeleza kuwa mbali na kuwa na mafaniko bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani ukosefu wa pesa jambo ambalo husababisha kujiendesha kwa michango binafsi.
"Fedha tunazozipata kutoka kwa wazazi, walezi na wafadhili ndio tunatumia na wakati mwingine hata hiyo michango haifikii malengo hiyo kupelekea kushindwa kufanya semina za mafunzo ya kiuongozi na utendaji kwa viongozi wa matawi ili waweze kujua majukumu yao na kufahamu mipaka ya kiutendaji" Alisema Mtataru.
Amefafamua kuwa ukosefu wa kadi za vijana hupelekea kuwa na kundi kubwa la vijana ambalo kwa namna moja ama nyingine wakiingia vyuoni ndio wanakutana na mambo ya siasana wengi kuwiwa kujiunga na chama hicho.
" Ukosefu wa kadi umepelekea kuwa n
a wanachama wa maneno na kushindwa kuwasajili ndani ya jumuiya kwani hakuna kadi za kuwapa pindi wanapohitaji" Alisema Mtataru.
Aidha ameleeza kuwa mbali na chanamoto hizo chama kinapaswa kutoa kadi 300 kwani itasaidia kuongeza wanachama kwenye jumuiya pia kuongeza kipato, pia kuweza kuwasaidia ruzuku ya kuendesha shughuliza senet.














0 Comments