Header Ads Widget

WAKULIMA WA MUHOGO WAOMBA ELIMU YA MARA KWA MARA

 



Na Mwandishi wetu, Ruvuma


Wakulima wa zao la muhogo kutoka kijiji cha Chimate kata ya Chiwinda Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa wameoiomba Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Naliendele kuwapa elimu ya mara kwa mara ya zao la muhogo hasa unapokaribia msimu wa upandaji wa zao hilo. 


Kauli hiyo wameitoa wakati wa siku ya mkulima iliyofanyikia kwenye shamba darasa la kijiji ambapo  Joshua Bugoro kulima wa kijij hicho alisema kuwa wakulima wengi ni wazee na hawana elimu ya kutosha hivyo ni vema elimu ikatolewa katika kipindi cha mwezi wa 12-1 ili kumpa nafasi mkulima kulima kwa vitendo baada ya mafunzo. 


“Sisi huwa tunapanda mihogo kuanzia mwezi wa 12 hadi wa kwanza tunapopata elimu kwa sasa huenda tukasahau tunaomba elimu hii itolewe mara kwa mara ili kuweza kutusaidia hasa sisi wazee”


“Haya mafunzo yana uhumuhimu mkubwa kwetu zao hili ni zao ambalo tegemezi kwetu na linatumiwa na wananchi wengi hivyo kujifunza mbinu mpya za upandaji zinaweza kuwa msaada zaidi na kuachana na upandaji wa mihogo kienyeji” 


Nae Selina Mmuya mkazi wa kata ya Chiwanda alisema kuwa elimu hiyo ni bora na inanda kubadilisha fikra na mitazamo ya wakulima wa zao hilo. 


“Elimu hii inaenda kubadilisha maisha ya wakulima wa kijiji hiki ambapo tunaimani kuwa watapata mazao mengi na kuisadia jamii hii ya wakulima ambayo haikuwa na uelewa wowote juu ya ulimaji wa zao la muhogo” alisema Mmuya


Kwa upande wake Afisa Kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tari  Naliendele Florah Liyumba alisema kuwa kitendo cha wakulima kushirikishwa katika mafunzo maalum ya zao la muhogo katika hatua zote hadi  uvunaji wa mbegu na kuchagua ipi inawafaa ni hatua kubwa.


“Tumekuja kuvuna mbegu za zao la muhogo na kuwaonyesha wakulima ubora wake na kuwapa elimu namna gani sahihi ya kupanda muhogo kwa nafasi ili waweze kuachana na upandaji wa mihogo wa kiasi ambao hauna tija kwao”alisema Liyumba 


Kwa upande wake Mtafiti wa zao la Muhogo kutoka Tari Naliendele Festo Masisila alisema kuwa Wakulima hawakuwa na ELIMU  yakutosha ya upandaji wa mihogo hali ambayo ilikuwa inapelekea kupata kiasi kidogo. 


Tutajitahidi kuendelea kutoa elimu kupitia mashamba darasa ili waondokane na upandaji wa mazoea wa asili na kuhamia katika teknolojia yenye manufaa kwao kwakuwapa vipimo sahihi namna bora ya ukataji wa mbegu za Muhogo na aina gani inafaa kwakula na kibiashara hasa mbegu bora zinazovumilia ukame na kinzani KWA magonjwa ya batobato na michirizi kahawia" alisema Masisila 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI