Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Tamasha kubwa la muziki wa dansi la 'Wafia Dansi' linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam Mei 28, mwaka ambapo bendi mbalimbali zikitarajiwa kutumbuiza katika Tamasha hilo liloandaliwa kwa lengo kutoa burudani kwa wakazi wa jiji hilo na viunga vyake.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Mwandaaji na Mratibu wa Tamasha hilo la Wafia Dansi, Benard James amesema lengo kubwa la tamasha ni kukuza muziki wa dansi ambapo kumekua na hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wa mziki huo tangu lilianza kufanyika katika mikoa mbalimbali lengo ikiwa ni kupunguza changamoto ambazo zimekua zikikwamisha kuendelea kwa mziki huo.
"Kwa miaka mingi mziki wa dansi umekua ukichukuliwa wa kawaida sana hata kupelekea waimbaji wake kukosa Soko, heshima na kutambulika kutokana na mazingira yaliokua yakitumika kuendeshea mziki huo ikiwemo kufanya show kwa kiingilio cha kinywaji, hii ilikosesha heshima sana mziki huu, lakini kwa sasa tumeamua kurudisha hadhi ya mziki wetu"amesema James.
Aidha, amewataka wadau na mashabiki wa mziki huo kujitokeza kwa wingi Ili kuweza kusapoti waimbaji wa mziki huo, ambapo pamoja na mambo mengine pesa zitakazopatikana zotakwenda kuzaa matunda ikiwemo kuwaenua wasanii wa mziki huo, pamoja na kukuza bendi ambazo zinafanya vizuri kwa sasa
Amesema kuwa, Tamasha hilo linatarajia kufanyika Mei 28 mwaka huu ambapo bendi 6 zitatumbuiza katika jukwaa moja katika ukumbi wa Gwambina lounge "tcc club" ambapo litapambwa na bendi maarufu ikiwemo Mapacha Music bendi, Bendi ya Waluguru Edition kutoka Morogoro pamoja Mjengoni Classic Bendi kutoka Arusha ambapo kiingilio ni shill10000 kwa kawaida na VIP ni shill 30000.
Kwa upande wake, Msaniii wa kundi la Mapacha Music Bendi, Josee Mara amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi na wakae mkao wa kula kwani kutakua na burudani za kutosha hivyo, wataweza kuenjoy sana kutokana nyimbo zitakazopigwa siku hiyo.
Amesema kuwa, tamasha hilo limekuja kwa wakati muafaka ikiwa ni katika jitihada za kuurudisha muziki wa dansi Tanzania huku akiahidi bendi hiyo itaweza kutambulisha nyimbo zake mpya katika tamasha, ambapo watu watafurahia sana katika usiku huo wa kipekee.
Akizungumza katika Mkutano huo Afisa Habari na Uhusiano wa Kampuni ya Mo Green International, Kessa Mwambeleko, ambao ni miongoni mwa wadhamini katika Tamasha hilo ambapo amesema licha ya kuwa wao wanashulika na masuala ya kilimo lakini wameamua kufadhili Tamasha hilo kwa lengo la kusapoti mziki wa dansi ambapo amewataka wadau wengine waende kushirikiana nao katika kukuza mziki wa dansi Tanzania.
"Tunaomba na wadau wengine waje kusapoti mziki wetu wa dansi Ili turudishe hadhi yake, huu mziki una historia kubwa nchini kwetu ni wakati muafaka kurudisha heshima ya mziki wetu"amesema Kessa.
Naye, Mkuu wa Masoko wa Gwambina Lounge, Sasilo Khalid ambao pia ni miongoni mwa wadhamini amesema wao wamejipanga vya kutosha katika Tamasha hilo, watu wengi atakaofika katika ukumbi huo wataweza kufurahia kutoka sehemu ilivyo.
"Watu hawatojutia kufika katika ukumbi huo kwani una mazingira mazuri vinywaji vya kutosha vizuri ambayo vitakwenda kuongeza Thamani ya usiku huo wa kipekee ambao unakwenda kurudisha hadhi ya mziki wa dansi katika Jijini la Dar es Salaam"amesema Sasilo.
0 Comments