Header Ads Widget

TIMU YA MBEYA KWANZA NA TANZANIA PRISONS ZA TUNISHIANA MISULI KUELEKEA KWENYE MCHEZO WAO WA MEI TANO MWAKA HUU

 .


Na Amon Mtega ,Matukio DaimaAPP,Ruvuma

Katika kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara Mei tano mwaka huu kwenye uwanja wa majimaji Songea kati ya Mbeya kwanza na Tanzania Prisons ambao umetafusiliwa kuwa ni dabi kutokana na timu hizo kutokea Jiji  moja la Mbeya zimetambiana kila timu kuwania alama tatu.


Akizungumza nahodha wa timu ya Mbeya kwanza Ramadhani Kimata amesema kuwa timu yake imejipanga vema na hakuna wasiwasi licha ya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo kufahamiana kwa kuwa zinatoka Jiji moja la Mbeya.



Kimata amesema kuwa timu ya Mbeya kwanza ambayo kwa sasa inatumia uwanja wa majimaji Songea Mkoani Ruvuma kama wanyumbani inafurahishwa na mashabiki wa Songea ambao wamekuwa mstali wa mbele kuipa nguvu timu hiyo kwa kuishangilia.


Kocha wa walindamlango (Goolkeepers) wa Mbeya kwanza Aswile Asukile amesema timu vizuri hivyo wanaimani kwenye mchezo huo kuibuka na ushindi na kuwa wao ndiyo wenyeji wa mchezo huo.



Naye nahodha wa timu ya Tanzania Prisons Benjamin Asukile amesema kuwa wao hawajaja kupoteza mchezo bali wamekuja kucheza na kuchukua alama tatu na kuwa yote kwa yote dakika 90 za mchezo zitaamua.


Hata hivyo kocha msaidizi wa timu ya Tanzania Prisons Shambani Mtupani amesema kuwa timu hiyo imekuja na kikosi chenye wachezaji 21 na kuwa wanamolari na mchezo wa kesho kukutana na watani zao.

 

 Ikumbukwe timu hizo zipo kwenye hali siyo nzuri katika msimamo wa ligi hivyo zinafulukuta kutaka kujinasua zisikutane na kisanga cha kushuka daraja.

           

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI