NA HADIJA OMARY _LINDI....
KATIBU wa Itikadi na Uwenezi Taifa Shaka Hamidu Shaka amefurahishwa na utekelezaji wa Mradi wa Tasaf wa Shamba la Minazi unaotekelezwa na walengwa wa kaya Masikini katika kata ya Kilangala Wilayani Lindi Mkoani Humo.
Mradi huo umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 15 huku walengwa 94 wakinufaika na mradi huo kwa kulipwa ujira wa muda.
Akizungumza Jana mai 30 katika Ziara yake ya kikazi ya siku mbili amewapongeza walengwa kwa juhudi kubwa yakuandaa shamba hilo ambalo limeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika familia zao .
Shaka amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia imeweza kuwapa fedha walengwa wa Tasaf kwa kila Halmashauri Nchi nzima ili kuweza kuwapa kaya masikini kwa kujiinua Kiuchumi.
Hata hivyo Shaka amesema fedha hizi za Tasaf ni jukumu la kila kiongozi kuhakikisha zinawafikia walengwa kikamilifu na sio vinginevyo kwa kuwa Serikali ya Mama Samia ipo macho katika kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kikamilifu katika maeneo yaliyokusudiwa .
" Nimefurahishwa na utekelezaji wa Miradi huu wa Tasaf wa Shamba la Minazi katika Mkoa wa Lindi niwaombe muendelee kusimamia kikamilifu miradi yote ya Serikali ambayo fedha zinaletwa kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu " Shaka .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amemuhakikisha Katibu mwenezi Taifa katika suala la Tasaf ndani ya Mkoa wa huo litasimamiwa kikamilifu katika Miradi na fedha zake ili kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa ipasavyo.
" Mimi pamoja na Viongozi wenzangu Mkoa Mzima wa Lindi tupo tayari kusimamia Ilani ya CCM kikamilifu katika Miradi yote na ndani ya Mkoa wangu walengwa wa Tasaf wamenufaika kikubwa katika kupata fedha hizo na wengi wanamiradi ya kujiendesha na kujipatia kipato Cha kila siku."
Kwa upande wao walengwa wa Tasaf akiwepo Christina Juma Mkazi wa kata ya Kilangala Manispaa ya Lindi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi huo ambao umekuwa msaada mkubwa kwa walengwa hao
Alisema mradi huo umeweza kuwasaidia walengwa kupata kadi za bima ya Afya , kuanzisha biashara ndogo ndogo na hata mashamba yanayowafanya kukuza kipato chao.
Rajabu Jafu mkazi wa kata ya Kilangala Manispaa ya Lindi "Tunajua Rais Samia anatujali na kutupenda wananchi wa Jimbo la Mchinga na sisi tupo pamoja nae katika kuhakikisha tunaisemea Serikali ya awamu ya sita vinzuri katika miradi mbalimbali ya Jimboni kwetu ."
0 Comments