Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amewapongeza wabunge wa Mkoa wa Iringa Kwa kuwa wamoja Katika kutetea ajenda za kimaendeleo zinazohusu Mkoa wa Iringa.
Akizungumza Mafinga Leo wakati wa Kikao cha wadau wa mazao ya misitu wanaojihusisha na uchakataji nguzo za Umeme kutoka Mkoa wa Njombe na Iringa, kikao hicho alihudhuria Mhe Waziri wa Nishati Mhe January Makamba ,Mhe Sendiga amesema Umoja ambao wameonesha kwenye kupigania suala la nguzo za Umeme kuendelea kununuliwa hapa hapa Nchini wamefanya Jambo la kizalendo sana kwani linaenda kuongeza mapato kwa serikali na Wananchi kwa ujumla. Vivyo hivyo amewataka kuendelea kufanya hivyo kwenye ajenda nyingine za ki mkoa .
Mhe Sendiga amesema kuwa Mkoa wa Iringa na Njombe ndio ambao wameuza nguzo zaidi ya asilimia 90 zilizotumika kusambaza Umeme nchini na walishangazwa sana kusikia hoja ya kuwa nguzo za ndani sio bora wakati tayari nguzo nyingi zimesimikwa Vijijini na zipo imara hivyo iweje Leo waseme Hazina ubora je tunaweza kuambiwa ni ubora gani wanao utaka hao Tanesko?
"Tukushukuru Mheshimiwa Waziri wa Nishati Kwa kufika Leo na kufanya maamuzi haya ambayo yana Afya kubwa Kwa uchumi wa mikoa hii miwili na Taifa"
Mhe Sendiga amesema baada ya suala la nguzo kumalizika wabunge hao wana wajibu wa kuendelea kusukuma ajenda ya Mkoa wa Iringa ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami toka Iringa hadi Ruaha Kwa ajili ya kuchochea kasi ya utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha .
Kwa upande wake Waziri Makamba amewatoa hofu wakulima wa miti na wachakataji wa mazao ya misitu kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wakala wa Umeme Vijijini (REA) wataendelea kununua nguzo za ndani.
Pia Makamba amemwagiza Kamishina wa Tanesko kuunda tume ya watu 12 itakayofanya kazi ya kuangalia ubora wa nguzo zinazo zalishwa katika Mikoa hii 2.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe Justin Nyamoga ameipongeza wizara ya Nishati chini ya Waziri January Makamba Kwa kuwa wizara sikivu Kwa kusikiliza kero kubwa ya nguzo za ununu na kuifanya kazi Kwa haraka .
Amesema ameona dhamira ya dhati ya wizara ya Nishati Katika kushughulikia na kumaliza kero kubwa ya ununuzi nguzo za ndani na kama msimamo wa Serikali ungekuwa ule wa kununua nguzo nje ya Nchi madhara yake yalikuwa makubwa Kwa uchumi wa Halmashauri za mikoa ya Iringa na Njombe.
Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga ameipongeza Serikali Kwa kushughulikia malalamiko ya wadau wa uchakataji nguzo za Umeme nchini na kuwa kilio Cha Nguzo hakikuwa ni kilio Cha wakazi wa Njombe na Iringa pekee bali kilikuwa ni kilio Cha Taifa zima hivyo agizo la Waziri wa Nishati January Makamba kuagiza nguzo za Umeme zinunuliwe hapa hapa nchini ni ukombozi mkubwa Kwa wakulima wa miti na wachakataji wa nguzo .
Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga amempongeza Waziri wa Nishati January Makamba Kwa kuwa msikivu na kutatua kero kubwa ya ununuzi wa nguzo za ndani.
0 Comments