Header Ads Widget

MBUNGE PROF. PATRICK NDAKIDEMI AENDELEA KUWAPAMBANIA WANANCHI WAKE.

 


NA WILLIUM PAUL.


MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof.Patrick Ndakidemi ameiomba Wizara ya maji kuhakikisha inatatua tatizo la maji linalowakabili wananchi wa kata za Kibosho kirima, Kibosho kati, Kibosho Okaoni, Kibosho magharibi, Mabogini.


Mbunge huyo pia amemuomba Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya maji kufika katika kata ya Uru kusini kuona jinsi gani wataweza kuwasaidia wananchi hao baada ya ripoti ya Mthibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kubainisha maji wanayokunywa wananchi hao sio salama na hayafai kwa matumizi ya binadamu.



Kauli hiyo ameitoa jana Bungeni wakati akijadili bajeti ya Wizara ya maji ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeomba kupatiwa Bilioni 657.9.


Prof. Ndakidemi alisema kuwa, katika kata ya Kibosho Kirima ambapo ndipo anapotoka imekuwa ikikabiliwa na tatizo la upatikanaji wa Maji safi na salama kwa muda mrefu sasa.



"Hii ni kata ninayotoka mimi kwa mwaka wote uliopita Bomba la nyumbani kwangu halijawahi kutoa maji  naomba Waziri utusaidie tupate maji najua unamipango mizuri hivyo nisaidie wale wananchi na mimi Mbunge wao tupate maji" alisema Prof. Ndakidemi.


Mbunge huyo aliendelea kubainisha kuwa, katika kata ya Kibosho kati na Kibosho Okaoni zenye vijiji 14 watu wameongezeka sana na kufanya mradi wa zamani uliokuwa ukihudumia wananchi wa maeneo hayo kutotosheleza mahitaji hivyo tunakuomba Waziri wa Maji uangalie hilo kuboresha miundombinu ili wananchi wapate maji.


Katika kata ya Kibosho Mgharibi vipo vijiji 8 ambavyo havijapata maji na kutumia nafasi hiyo kuiomba Wizara kuviangalia kwa jicho la huruma kumtafuta chanzo kipya ili kuwafikishia wananchi hao maji.


Kati ya Mabogini vipo vijiji ambavyo tangu nchi ipate uhuru vilikuwa havina hata maji ya mfereji hivyo ameiomba Wizara kuhakikisha navyo vinafikiwa na huduma ya maji safi na salama.



"Kata ya Old Moshi mashariki imepewa milioni 400 za mradi wa Maji lakini changamoto ipo kwenye manunuzi yaboreshwe hii ni pamoja na kata ya Mbokomu na hata kata ya Kimochi iloyopatiwa milioni 500 na kazi imeshaanza" alisema Mbunge huyo.


Akizingumzia swala la Uru kusini, Prof. Ndakidemi alisema kuwa katika ripoti ya Mthibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) ilieleza kuwa maji yanayotumiwa na wananchi wa kata hiyo hayafai kwa ajili ya matumizi ya binadamu hali ambayo imepelekea wananchi kuogopa na kuingiwa na hofu na kuiomba Wizara ya maji kufika na wataalam kuangalia ili kuwasaidia wananchi hao.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS