Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Hashim Komba amewataka Kamati ya Pembejeo za kila wilaya na Vijiji kuhakikisha Pembejeo ambazo zimeletwa na Rais Samia Suluhu Hassan zinawafikia wakulima wote na bule bila Malipo yoyote.
Akizungumza Leo katika kikao Cha maandalizi ya Ununuzi wa ufuta Mh Komba amesema kwa mwaka huu katika Mkoa wa Lindi maghara yote yatafunguliwa Tarehe 28/5/2022 na kuwaomba wakulima kupeleka mazao yao magharani .
" Kila mkulima kuhakikisha analinda Ubora wa ufuta wetu kwa kuufanyia Usafi ufuta wako kabla ya kufika gharani na niwaombe wakulima wangu kulinda Soko Letu ili wanunuzi wapate kununua mazao yetu yaliyosafi na yenye Ubora"Mh Komba
0 Comments