Baraza la Waislamu (BAKWATA Mkoa wa Mwanza wameshiriki chakula cha Eid Elfitr na watoto yatima, wanawake wajane pamoja na watoto na vijana wanaofanya kazi mtaani huku jambo hilo likitajwa kuwa ni moja ya nguzo ya kiimani.
Akizungumza kwa niaba ya Baraza hilo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke ameeleza kula chakula pamoja na watoto hao ni jambo lenye baraka pamoja katika wislamu kukaa na watoto yatima majumbani ni jambo ambalo ni bora na lenye kuleta tija na baraka kwa Mungu kuliko kuwalea kwenye vituo vya kuwalelea.
"Mtume anasema mtu yeyote yule mwenye kuishi pamoja na yatima basi atakaa nae pamoja peponi hii ni fursa muhimu sana kwa waislamu na wasiokuwa waislamu" Alisema Kabeke.
Kabeke ameeleza kuwa kushiriki chakula na watoto yatima ni jambo ambalo linapaswa kufanyika kila wakati lakini kwa sasa jamabo hilo halifanyiki kama zamani ambavyo lilikuwa likifanyika hususani pale wazazi wanapofariki vikao vilifanyika ili kufahamu watoto walioachwa wataishi katika mazingira yapi ila kwa sasa hali imekuwa tofauti.
" Lakini sasa waislamu wengi tumekimbia kuwalea watoto majumbani na tumeamua kuwakusanya katika vituo vya kulelea" Alisema Kabeke.
Ametoa wito kwa waislamu wenye uwezo na wasio na uwezo kusaidia wale ambao wanawalea watoto kwenye vituo.
"Nasema wawasaidie kwa sababu jamii yenyewe na baadhi ya waislamu wameliacha jambo hilo ambalo ni jema" Alisema Kabeke.
Msitaiki meya wa jiji la Mwanza Costantine sima ambaye pia alikuwa mgeni rasmi amelipongeza Baraza hilo kwa kuliona jambo kwani ni jambo ambalo ni la kibinadamu.
Sima amesema kuwa serikali inalitambua kuwa wanaowajibu wa kuhakikisha kundi hilo maalum linalelewa linatunzwa na kulindwa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Rock Solution limited Zacharia Nzuki ambaye ni mhisani wa shughuli hiyo ameeleza kuwa jambo wamekuwa wakifanya mara kwa mara shughuli hiyo na sio kwa waislamu peke yao na hata kwa watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu.
" Ni jambo ambalo tumekuwa tukijitolea kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu sehemu mbalimbali kutokana na watoto hao kuwa wengi" Alisema Zacharia.
Baadhi ya watoto walioshiriki katika chakula hicho wamelishukru baraza hilo la waislamu na kuwataka kuendelea na moyo huo kwani hawajawahi kupata msaada kama huo kutoka kwa mashirika yeyote wala watu binafsi.
Kwa upande mwingine watoto hao wanaoishi mtaani wameeleza kuwa kutokana na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa wazazi wao walezi ndio chanzo cha wao kuishi mazingira magumu.
Watoto hao wameeleza kuwa wamekuwa kutokana na kunyimwa chakula kulazwa nje kupigwa kila siku pamoja na kunyang'anywa mali pindi wazazi wanapofariki kumewapelekea kusafiri kutoka sehemu mbalimbali na kuja katika jiji la Mwanza kutafuta maisha lakini mwisho wake wameishia kutumia madawa ya kulevya.
" kiukweli mateso tunayoyapata ni makubwa tukiwa huko nyumbani ndugu wenyewe wanatutenga hatutaki pindi tu wazazi wanapofariki maisha yetu yanakuwa ya shida ndio maana tunatoroka na kuja huku yani nyumbani sio salama na huku sio salama" walisema watoto hao.
Hata hivyo wametoa wito kwa watoto wanaoishi nyumbani na wazazi wao vizuri kuendelea kuwaheshimu na wasitani maisha ya mtaani kwani maisha ya huko ni magumu.
" Niwashauri watoto walioko majumbani wasitamani maisha ya huku maisha ni magumu sana tunaangaika pa kulala tena hususani katika kipindi cha mvua" walisema watoto hao.
0 Comments