Header Ads Widget

ACT WAZALENDO CHAJA NA MKAKATI WA KUWEPO KWA TUME HURU YA UCHAGUZI

 


Na Ibrahim Kunoga,Matukio DaimaAPP Tanga.

Chama cha ACT Wazalendo kimepanga kufanya jitihada za kuhakikisha kunakuwepo na tume huru ya uchaguzi kwanza kabla ya kuelekea kwenye katiba mpya.

Haya yameelezwa na naibu msemaji wa sekta ya elimu wa chama hicho bahati Chirwa wakati wa kikao cha viongozi wa mkoa.

Bahati amesema jitihada za  viongozi wao ni kupigania  tume huru ya uchaguzi kuelekea katiba mpya.

Amesema lengo la chama cha siasa ni kushika dola bila kuwa na tume huru ya uchaguzi hawawezi kufanya uchaguzi utakaopelekea kushinda.

Ameongeza kuwa kiongozi wa chama chao cha ACT Wazalendo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kunakuwa na tume huru ya uchaguzi na mpaka viongozi wa dini nao wamekuwa wakizungumzia kuwa na tume huru.

"Kiongozi wa chama chetu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuna kuwepo na tume huru ya uchaguzi ili kuwepo na siasa za kidemokrasia pamoja na viongozi wa dini nao wakisisitiza swala zima la tume huru;Alisema Bahati.


Sambamba na hayo kamati ya chama hicho mkoani Tanga imekutana kuangalia namna bora ya kuhakikisha wanajipanga kupata wanachama wapya na mikakati ya kujidhatiti zaidi.

Akizungumza wakati wa kikao mzee wa chama hicho Ally Sungura ameeleza kuwa kitu cha msingi wanachosisitiza ni kuwa chama bado kipo imara ingawa kilikuwa na ukimya wa muda mrefu kutokana na mwenendo wa siasa hapo awali.

Chama kipo na tumejipanga  na tunatangaza rasmi kwamba tutasikika kwenye maeneo yote kuanzia mashina, kata, jimbo na mkoa kwa ujumla kupata wanachama wapya na wengi katika kujiandaa na uchaguzi wa serekali za mitaa, 

Sungura amesema tayari wameshakamilisha taratibu zote za kukitangaza chama ndani ya mkoa wa Tanga kwa Vitendo.

"Naomba wanachama waamini chama kipo na muda sio mrefu yataanza matukio makubwa ya ujenzi wa chama bila kupumzika ya kuanzia sasa hadi uchaguzi wa serekali za mitaa utakapoanza  hadi wakati wa uchaguzi ;Alibainisha Sungura.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI