Na Matukio DaimaAPP, Mtwara
Watafiti wa program wa ufuta kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania kituo cha Naliendele wametoa mafunzo kwa watafiti wenzao wa mazao mbalimbali kutoka kituoni hapo ili kufahamu namna tafiti za zao LA ufuta zinavyofanyika sambamba na upandaji shambani.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Tari Naliendele Dr Furtunus Kapinga alisema kuwa mafunzo hayo yamepangwa kwa awamu ili watafiti waliopo katika kituo hicho waweze kufahamu nini kinafanyika kwenye zao la ufuta na mazao mengine.
Alisema kuwa tumepanga kila msimu watafiti watapita kujifunza na kuona nini wenzao wanafanya hii itasaidia kujua tafiti zinafanywaje.
"Kazi yetu kubwa no kufanya tafiti kwakuwa tunaowatafiti wa mazao mbalimbali tunalazimika kuwapitisha kwa kila zao ili wafahamu nini kinafanyika na nini kinahitajika ikiwa ni sehemu ya kushauriana na kujifunza zaidi?" Alisema Dr. Kapinga
Mratibu wa zao la ufuta kitaifa Joseph Nzunda alisema kuwa mafunzo hayo yataongeza uelewa na ufahamu kwa watafiti wengine juu ya zao LA ufuta.
"Unajua tafiti nyingi zinalenga kumuinua mkulima ili aweze kupata mbegu bora na aweze kulima kwa Tina kwakupata mazao mengi zaidi pia Mbali na kupata mafuta kwenye ufuta lakini unapata pesa no zao ambalo linaweza kutotoa kwenye umasikini endapo utalitilia mkazo" alisema Nzunda
Kwa upande wake mtafiti mstaafu wa zao la ufuta Dr Omary Mponda amesema kuwa amefurahishwa na jitihada kubwa za kitafiti zinazoendelea kufanyika katika kitengo cha Ufuta.
Nimefurahi kuja hapa niliondoka miaka mitatu iliyopita lakini vijana waliopo wanafanyakazi kubwa zaidi na inaonekana hizi tafiti zikiendelea hivi tunaweza kufika mbali zaidi natambua serikali imeona mchango wa tafiti na imeongeza bajeti ni jambo la msingi Rais Samiah Suluhu ameona na amelikubali" alisema Dr Mponda
0 Comments