WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa wasiwachague viongozi wanaotumia rushwa au umaarufu wao kuwania uongozi.
Hayo yalisemwa Wilayani Mkuranga na Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Abdulrhaman Kinana wakati wa ziara yake ya siku moja kutembelea mkoa huo.
Kinana alisema kuwa viongozi hao hawafai na wanachama wanapaswa kuchagua wale ambao watawaletea maendeleo.
Alisema kuwa kabla hajateuliwa mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan alitakiwa asimamie uchaguzi wa ndani ya chama ili kusiwe na uonevu ili wale wenye sifa wapate hizo nafasi lakini siyo kwa njia za rushwa.
"Kabla mwenyekiti hajaniteua aliniita na kunipa maagizo kwanza nisimamie uchaguzi wa CCM nihakikishe uchaguzi uwe huru na haki maelekezo njia iliyo huru na haki,"alisema Kinana.
Alisema viongozi wanaosimamia chaguzi hizo wasioneane haya kwani wanawajua wanaotoa fedha au wanatumia njia nyingine kuwachafua wenzao.
"Mtu anazushiwa mambo ambayo hayapo kamati siasa mkoa na Wilaya pateni taarifa zilizo sahihi mtu asidhulumiwe tunataka viongozi waadilifu hapana kubebana ili upate uongozi unatengeneze uongozi matawi yako ili ushinde kwa hali hiyo tutafanya ushindwe,"alisema Kinana.
Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdala Ulega alisema kuwa wanashukuru kwa ziara hiyo Kijiji cha Mwanambaya ameacha historia amepata elimu kupitia Kinana na aendelee kumsaidia Rais.
Ulega alisema kuwa ajenda moja wanamshukuru Rais wilaya imepata madarasa mengi shule, miradi ya miundombinu ilikuwa ni ndoto lakini sasa zinapitika Vikindu hadi Tundu Songani ujenzi wa stendi ya mabasi ya Kusini stendi itaitwa Samia Suluhu Hassan mkoa wanaomba mradi ukamilike watu wapate ajira.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno alisema wanakumbusha kauli iliyotolewa na aliyekuwa Rais Hayati Dk John Magufuli akiwa Chalinze anatamani Chalinze iwe wilaya au kichama.
Naye mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuupatia mkoa huo fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kunenge alisema kuwa mkoa umepata miradi mingi ikiwemo Ile ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ule wa kuyatoa maji mto Rufiji ili kuyasambaza ili kuondokana na changamoto ya huduma hiyo.
0 Comments