Header Ads Widget

TANZANIA KWA KIPINDI KIREFU HAINA TAKWIMU SAHIHI ZA NYUMBA -RIDHIWANI

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

NCHI ya Tanzania kwa Kipindi kirefu imekuwa Haina takwimu sahihi za Nyumba na hali ya matumizi ya nyumba au majengo hali iliyokuwa haitoi taswira  ya hali halisi ya Makazi na ukuaji wa miji hapa nchini .


Hayo yameelezwa leo Jijini hapa na Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete katika ufunguzi wa kikao kazi cha wadau juu ya maandalizi ya Sensa ya Majengo .


Amesema kwa mara ya kwanza nchi ya. Tanzania itakusanya taarifa za Nyumba/ Majengo yote yaliyopo nchini  katika Sensa ya Watu na makazi ya 2022 ambapo kukamilika kwa zoezi hilo itasaidia kupatikana kwa taarifa na kitakwimu za Majengo zilizo sahihi na za wakati.


"Madhumuni Makuu ya kufanya Sensa ya Majengo ni kukusanya taarifa za Majengo yote nchini ili kupata Takwimu za Majengo na kupima hali ya umasikini usio wa kipato kwa Wananchi ili kuwezesha kutathimini na kupanga Maendeleo ya miji na wakazi wake,"amesema


Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Allan Kijazi amesema ili zoezi hilo lifanyike kwa ufanisi na liwe mfano wajitahidi kupitia maoni yatakayosaidia zoezi kufanyika kwa kasi kubwa na wasitegemee Wizara au Serikali peke yake.


Pia Naibu Waziri  huyo amewataka wadaau kutoa elimu kwa Watanzania ili waweze kushiriki katika zoezi zima kwani kumekuwepo na maneno mengi hali inayowaogopesha Wananchi kushiriki zoezi hilo huku akiwataka wadau hao kushiriki katika vikao na wasisubiri vikao vya kuitwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI