Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema kuna umuhimu wa kuangalia upya namna Bora ya kupeleka mikopo katika elimu ya ufundi walau kwenye Diploma kwa vyuo vya Ufundi na Ujuzi.
Prof mkenda ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na bodi ya mikopo (HELSB) ambapo amesema kuwa waombaji wengi hukosa mikopo wanayoomba kutokana na kutofata maelekeo pamoja na kutoambatanisha taarifa zote zinazomhusu muombaji.
Amesema taaluma za ujuzi ndizo zinazohitajika Sana kwenye ajira kwani kilio Cha Watu wengi ni ajira na sehemu yenye ajira zaidi ni sehemu ya ujuzi na ufundi Mwaka mpya wa fedha ujao sio Mwaka huu tutapeleka fedha kwa ajili ya wanafunzi wa ufundi kuweza kupata mikopo.
Katika hatua nyingine amesema Katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG Charles Kichere aliyoitoa hivi karibuni ilieleza kuna shida Katika Bodi ya mikopo hasa katika zoezi zima la ugawaji wa mkopo Ni kutokana na wanafunzi wenyewe kuandika taarifa zisizosahihi na wengine kuchelewa kuomba mkopo.
Amesema wamezungumza na Bodi na wamepata taarifa kuwa tatizo lilikuwepo huko nyuma na Sasa kuna maboresho makubwa mpaka Sasa na juhudi za kuboresha zitaendelea .
"Kwa sababu mkopo unatolewa kwa taarifa zinavyotolewa na wanafunzi wanaomba mkopo hivyo mwanafunzi akichelewa au ukitoa taarifa sio kamili anaweza kukosa mkopo ingawa una vigezo vya kupata mikopo," amesema
Na kuendelea"Tumekubalina na Bodi ya mikopo kunaendelea kuchakata na kila mtu ambaye GAC ameona amekosa mkopo na aliyestahili kupata mkopo kuwe na taarifa itakayokwenda bungeni na kukukutana kamati ya bunge na hapo kutakuwa na fursa ya kuhabarisha Umma zaidi," amesema.
Hata hivyo amesema Ukaguzi huo ulifanyika Kama miaka miwili iliyopita na maboresho yamefanyika na maboresho yanaendelea ili kuhakikisha wale wote wanafunzi wanaostahili kupata mkopo waweze kupata mkopo.
Pia Prof Mkenda alitoa wito kwa wanafunzi wanaomba mkopo pindi wanapoomba mikopo kuandika taarifa iliyosahihi kwani ukikosea kitu kimoja na bila ushahidi unaweza kukosa na wanapokwama watoe taarifa kwa Bodi ya mikopo na Bodi imesema watanitahidi kushughulika kwa haraka sana
Aidha,prof mkenda amesema wizara ya elimu sayansi na teknolojia imetenga bajeti kwajili ya wanafunzi wanaofanya vizuri upande wa sayansi watapata udhamini wa masomo(scholarship) huku akiyataka makapuni mbalimbali nchini kutoa fursa kwa wanafunzi ili kuwatia moyo wasome kwa bidii na kupata ufaulu mzuri.
Kwa upande wake prof.Hamisi Dihenga Mwenyekiti wa Bodi ya mikopo (HELSB) amesema wao kama bodi nikuhakikisha kwamba utaratibu wa kutoa mikopo ni utaratibu unao eleweka pamoja na kuhakikisha mikopo wanayotoa inawalenga wale wanaostahiki kupewa.
MWISHO.
0 Comments