Header Ads Widget

ROYAL TOUR KUZINDULIWA KITAIFA ARUSHA NA RAIS SAMIA.


Na Teddy Kilanga Matukio Daima APP Arusha.

Serikali mkoani Arusha imempongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuzindua filamu ya Royal iliyoleta matokeo chanya katika sekta ya utalii kwa kuongeza watalii kutoka 620,549 hadi 922,692 kwa mwaka 2020/2021.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amesema watalii wa ndani ni 562,549 hadi 788,933 kwa kipindi cha mwaka 2020/2021.



Aidha amesema kuwa kupitia matokeo hayo chanya ya Royal tour iliyozinduliwa nchini Marekani mnamo Aprili 18,2022 na kitaifa itafanyika jijini Arusha Aprili 28 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.



"Kwa hapa nchini kwetu uzinduzi wa filamu hii yenye lengo la kuvutia watalii wengi na wawekezaji nchini utafanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa AICC ambacho ni kitovu cha utalii,"amesema.



Amebainisha katika uzinduzi huo wanatarajia  kuwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa,mabalozi,wawekezaji,wadau wa utalii na uhifadhi,wafanyabiashara pamoja na wananchi kutoka  mikoa ya jirani hasa kilimanjaro,Tanga,Manyara,Mara na Arusha yenyewe.



Mkurugenzi wa masoko wa AICC,Mkunde Senyagwa Mushi,kupitia uzinduzi huo unarotarajiwa kufanyika jijini Arusha wataandaa kulingana na viwango vya kimataifa ili uzinduzi uweze kwenda vizuri na kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi zote katika kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan.



Kwa upande wake kamishna msaidizi utalii kutoka TAWA,Segoline Tarimo amesema wako bega kwa bega na Rais Samia Suluhu Hassan kwa katika uzinduzi wa filamu hiyo kwani imeleta matokeo chanya nchi hivyo watahimarisha miundombinu mbalimbali  ya utalii kwa ajili ya wageni.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI