Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI KIKWETE KUMALIZA MGOGORO ULIODUMU ZAIDI YA MIAKA MITANO


NAIBU waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (MB) anatarajia kufika Keko Machungwa  Manispaa ya Temeke kumaliza Mgogoro uliodumu kwa miaka mitano bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu, baada ya familia ya Ali Akida kudai eneo hilo ni Mali yao baada ya wananchi kuvamia bila utaratibu


Naibu waziri amesema serikali ya awamu ya sita chini ya mama Samia Suluhu Hassani itahakikisha migogoro inapungua au kuondoka kabisa kwenye umiliki wa Ardhi nchini, amesema ofisi za wizara zipo wazi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi bila kuwabagua "nitafika kwenye eneo la mgogoro kufanya maamuzi na nitahakikisha kila mmoja anatendewa haki" alisema



Aidha, akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wa hadhara Kamishna Msaidizi wa Ardhi Nyumba na Makazi Mkoa wa Dar Es Salaam Idrisa Kayera amesema wizara imeamua kufika katika eneo lenye Mgogoro na kubaini changamoto mbalimbali zilizojitokeza hasa baada ya wananchi kuomba kufanyiwa urasimishaji ili kumiliki Ardhi kihalali, ameongeza kuwa sheria na Ardhi namba 4 na 5 inazungumzia jinsi Ardhi inapotwaliwa na inaeleza pia uwazi kuhusu umiliki wa kipande cha Ardhi na kila mwananchi anapaswa kufuata sheria hizo ili kutojiingiza katika migogoro isiyo ya lazima


Kamishna amewataka wananchi wa eneo hilo kufuata taratibu za umilikishwaji Ardhi ukiwa ni pamoja na uwepo wa nyaraka muhimu "kila mmoja anapaswa kuonesha namna alivyolipata, hii nyaraka ni muhimu sana, kama umenunua onesha hati halali ya mauziano, na kila mnunuzi wa kipande cha Ardhi azingatie uwazi wa nyaraka halali" alisema 


Naye Zainabu Milinga mkazi wa Keko Machungwa ameiomba serikali kumaliza haraka mgogoro huu uliodumu muda mrefu, amesema kufika kwa kamishna katika eneo la mgogoro ni jambo kubwa la kupongezwa na kutoa salaam kwa Raisi Samia Suluhu Hassani kwa kuwagusa wananchi wa chini ambao walikuwa na matatizo sugu ya Ardhi lakini hivi sasa tunashukuru  viongozi wanatufuata kutuhudumia kwa wakati








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS