Header Ads Widget

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE UJUMBE WA MWENGE



Na  Amon Mtega MATUKIO DAIMA APP RUVUMA 

        MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo ya kutolea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru ili ujumbe huo uweze kuwafikia kikamilifu.


 Wito huo ameutoa wakati akizungumza na vyombo vya Habari Mkoani humo juu ya kuwasili kwa Mwenge wa Uhuru Aprili 08 mwaka huu ukitokea Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe na kupokelewa katika Kijiji cha Lituhi Wilaya ya Nyasa Mkoani humo.


 Ibuge amesema kuwa Mwenge huo utakapokuwa Mkoani humo utakimbizwa  kilomita 1,052.3 katika Wilaya tano zenye Halmashauri nane na utapitia miradi 62 yenye thamani zaidi ya Shilingi Bilion 5.2 huku kati ya miradi hiyo miradi 29 yenye thamani ya Shilingi zaidi ya Bilion 2.6 itafunguliwa na miradi 5 yenye thamani ya Shilingi zaidi ya Bilion 1.511 itawekwa jiwe la Msingi na miradi 28 yenye thamani ya Shilingi zaidi ya Bilion 1.082 itatembelewa na kukaguliwa pamoja na kugawa vifaa mbalimbali.


 Mkuu huyo amesema kuwa Mwenge huo wa Uhuru umebeba ujumbe maalum usemao Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo ,shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo  tuyafikie maendeleo ya Taifa hivyo Wananchi wanatakiwa kuipata kaulimbiu hiyo ili muda wa sensa ukifika waweze kushiriki kikamilifu.

 

 Amesema kuwa pamoja na kaulimbiu hiyo lakini mwenge wa Uhuru utapita kuelimisha na kuhamasisha jamii ya wanaruvuma kuzingatia Lishe bora ,Mapambano dhidi ya Rushwa , Mapambano dhidi ya VVU, UKIMWI, Mapambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria ,pia na kutakuwa na mabanda ya Elimu kuhusu UVIKO -19 na uchanjaji kwa ambao bado.

                   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI