Header Ads Widget

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWATAKA WAKAZI WA MKOA HUO KUPUUZA UWEPO WA SHULE YA NYASI

  



Na Amon Mtega,Matukio DaimaAPP

    Ruvuma.

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia generali Wilbert Ibuge amewataka wakazi wa Mkoa huo pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kupuuza taarifa ya kuwepo kwa shule ya msingi Litapatile ,katika Halmashauri ya Madaba Mkoani humo  inayo daiwa darasa lake  limejengwa kwa miti na kuezekwa  nyasi kisha kutumika kama darasa la kusomea wanafunzi.


 Akizungumza na vyombo vya Habari vya Mkoani humo kufuatia taarifa ya kudai kuwepo kwa Shule hiyo ambayo  imerekodiwa kwa njia ya  video kisha kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii mkuu huyo amesema huo ni uzushi uliofanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kuuchafua mkoa na Serikali yake kwa ujumla.


Ibuge amesema kuwa eneo la Litapatile ambalo hadi kulifikia kutoka Kijiji cha Luhimba kata ya Mtyangimbole ni zaidi ya Klometa 48 na hakuna miundombinu ya barabara  hivyo haipo  shule ya Msingi na wala shule Shikizi bali ni  eneo la kufanyia shughuli za kilimo na malisho ya mifugo .


Hivyo amesema kuwa suala la kujenga kibanda cha miti kisha kuezeka nyasi na kutumia kama darasa la wanafunzi  halikubaliki na kuwa wakazi wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo hayo wanatakiwa kuwapeleka watoto wao kwenye shule ambazo zipo kwa muujibu wa kanuni na zinatambulika na Serikali akiwemo shule ya Msingi iliopo kwenye Kijiji chao cha Luhimba.


Amesema kuwa kibanda hicho kilichofanyika kama shule kinadaiwa  wanafunzi wake wamekuwa wakifundishwa na mtu ambaye haifahamiki kama anataaluma ya uwalimu au laa  na inasemekana  amekuwa akilipwa posho  na Wazazi wa wanafunzi hao ambopo  lina wanafunzi wasiopungua 13 na wapo hadi darasa la tatu jambo ambalo halikubaliki kwa mujibu wa kanuni.


Akitoa msimamo wa Serikali Mkuu wa mkoa huo Wananchi wote wa eneo hilo waliofanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua na kwa kuwa wamekuwa na dhamila ya kuwanyima watoto wao wasipatiwe Elimu iliyo bora kutokana na uzembe wa Wazazi  hao.


 Aidha amewataka wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi na Maafisa tarafa wa mkoa huo kuyasimamia kikamilifu maeneo yao wanayoyaongoza ili kudhibiti vitendo vibaya kama hivyo vya uanzishwaji wa shule bila utaratibu.


      Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI