Na Editha Karlo,Matukio Daima APP Kigoma
Tatizo la mimba kwa wanafunzi na ndoa za utotoni kwa Mkoa wa Kigoma bado ni changamoto kubwa hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
Hayo yamesemwa na kaimu ofisa Elimu wa Mkoa wa Kigoma David Mwamalasi kwenye uzinduzi wa shindano la uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za msingi za Mikoa ambayo shirika la word vision Tanzania linafanya kazi.
Alisema lengo kuu la shindano hilo ni kupinga mimba na ndoa za utotoni ambazo huathiri safari ya masomo kwa watoto wa kike na kushindwa kufikia ndoto zao katika maisha.
Alisema mwaka 2021 kwa Mkoa wa Kigoma watoto wa kike waliotoroka na kuacha shule jumla walikuwa 6,799(msingi 6123 na sekondari 676),Pia watoto wa kike kwa upande wa sekondari kuanzia january hadi february 2022 walioacha shule kwa kupata mimba ni wanafunzi 28.
“Shindano hili la insha litasaidia kuwajenga watoto wa kike kutokudanganyika kuingia katika mitego ya kupata mimba pamoja na ndoa za utotoni kwaajili ya ustawi wa Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla”
Aliongeza kwa kusema pia ili kupambana na tatizo hilo serikali ya Mkoa imekuwa ikiendelea na jitihada mbalimbali za kupambana kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo kwa kukaa vikao na wadau mbalimbali wa elimu,waalim,wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la Word vision Tanzania Vicent Kisula akisoma hotuba yake kwenye zoezi la uzinduzi wa mashindano ya uandishi wa insha kupinga mimba na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Naye mwakilishi kutoka shirika la Word vision Tanzania Vicent Kasuga alisema kuwa mategemeo yao shindano hilo la uandishi wa insha wanafunzi 100,000 watashiriki ambalo litafanyika katika shule 544 za msingi.
Kasula alisema kuwa katika shindano hilo watakuwa na washindi katika ngazi ya Wilaya,Mkoa pamoja na Kitaifa alisema washiriki wa shindano hilo ni wanafunzi wa darasa la sita na saba kwa shule za serikali tu.
Alisema pia shindano hilo litafanyika katika mikoa 16 ambayo shirika la Word vision Tanzania linafanya kazi Mikoa hiyo ni Kigoma,Kagera,Dodoma,Singida,Shinyanga,Tabora,Simiyu,Arusha,Manyara,Iringa,Morogoro na Tanga.
Naye mgeni rasmi katika zoezi la uzinduzi la mashindano ya uandishiwa insha kupinga mimba na ndoa za utotoni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alilipongoza shirika la word vision Tanzania kwa heshima kubwa waliyoipatia Mkoa wa Kigoma kwa kuzindua mashindano hayo mkoani humo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe alisema kuwa analipongeza shirika la word vision Tanzania kwa kuanzisha shindano hilo ambalo lina lengo la kumlinda mtoto wa kike pamoja na wa kiume pia.
‘’Kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa ya kuhakikisha tunamlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utotoni ila kwa umoja wetu naamini hili tunaliweza’’Alisema
Aliwataka wazazi na walezi pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kuungana katika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto na jinsi y kujilinda na ukatili na kutoa taarifa pale mtoto anapo fanyiwa ukatili.
‘’Siku hizi maadili yamebadilika ni jambo la kawaida kusikia baba kabaka mtoto wake wa kumzaa,na haya yote yanatokea kwasababu mbalimbali ikiwemo mila na desturi,umaskini pamoja na kukosa elimu viongozi wa dini na wadau wengine tusaidiane kufikisha elimu kwa jamii ili tuweze kuwalinda watoto wa kike na hata wa kiume pia’’Alisema Mkuu wa Mkoa
Wadau mbalimbali wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa uzinduzi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za msingi wa darasa la sita na saba.
0 Comments