Header Ads Widget

CHAKULA CHA UBONGO

 


Na  Peter Msigwa

43% ya Ndege wale waliopaswa  kuruka hawawezi kuruka, nchini  New Zealand. 

Idadi kubwa ya hawa ndege wamelemaa kwa sababu kumekuwa na upungufu mkubwa wa wanyama wanaokula wanyama Yaani (Predators)


Tatizo hili limekuwa kwa muda mrefu kiasi kwamba ndege ambao asili yao sio kujenga viota ardhini wamekuwa wanajenga viota vyao ardhini. 


Baada ya kupita muda Ndege hawa hata wale wenye asili ya kuruka wamelemaa kwa sababu hawapati challenge kutoka kwa predators.


Tatizo hili lliilazimu serikali kuingiza Nyoka na Panya kutoka sehemu nyingine Duniani ili waweze kuwachangamsha hawa ndege waweze kuruka


Moja ya jambo linalochangia umaskini katika bara la Africa ni chakula cha bure, Kinachotolewa na wazazi , wajomba na akina shangazi kwa vijana wenye umri  na  uwezo wa kufanya kazi na hatimaye kinawalemaza.


Katika Bibilia kitabu cha kutoka kila kijana aliyefikisha miaka ishirini alipaswa kwenda vitani.  Kwa maana ya kuwa ni mtu mzima anayeweza kupigana na kufanya maamuzi.

 

Hata hapa kwetu Tanzania kijana wa miaka 16-18 anajiunga na Jeshi na anakabidhiwa bunduki kwa ajili ya kuilinda nchi yake.

Na akienda vitani akikutana na adui huwa haulizi kwa baba au mama yake kama anaweza kumuua adui !

Maamuzi anakuwa nayo yeye.


Kama nchi inaweza kumwamini na kumkabidhi Bunduki kijana wa miaka

18, kwa nini ?

Leo majumbani mwetu tuna vijana wa miaka 20, 25,27,30 ambao tunaendelea kuwapa chakula cha bure (Free food)


Kijana akipata chakula cha bure hawezi kufikiri akishindwa kufikiri hawezi Kuwa productive.


Hata kuku kuna wakati huwa anaachana na kufukuza vigaranga vyake.


Nini maoni yako.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI