Header Ads Widget

ASKOFU NDIMBO WA MBINGA AIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA 6 KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI.

 


NA AMON MTEGA, _ MBINGA.


ASKOFU John Ndimbo  wa kanisa la Romani Katholiki  Jimbo la Mbinga Mkoani ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya kwa Wananchi wake ili kuwakinga na maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa malaria.


Pongezi hizo amezitoa wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Gabriel kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma wakati mwenge huo ulipoweka jiwe la msingi kwenye kituo hicho kitakacho garimu zaidi ya sh.Milioni 90 hadi kitakapo kamilika.


 Askofu Ndimbo amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan  imekuwa ikizingatia masuala ya Afya kwa Wananchi wake kwa kuwajengea Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati jambo ambalo litawasaidia Wananchi hao kuendelea kuwa na Afya njema.



Amesema kituo hicho cha Afya kikikamilika kitapunguza msongamano kwa wagonjwa ambao huwa unajitokeza katika Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga mji (Mbuyula)pindi wanapoenda kupatiwa huduma za Afya na kuwa kituo hicho kitakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo ya upasuaji.


Hata hivyo Askofu Ndimbo licha ya kuipongeza Serikali kwa kujali huduma za Afya katika Sekta zote ikiwemo za taasisi binafsi bado umeupongeza ujumbe wa mwenge uliyobeba mahudhui mbalimbali ikiwemo suala la kujitokeza kwenye kuhesabiwa (Sensa)muda utakapofika.




 Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kituo cha Afya cha Mtakatifu Gabriel kinachomilikiwa na misheni ya Mbinga amempongeza kwa Askofu huyo kufuatia kituo hicho na kuwa watakaokuwa wakipatiwa huduma ni Wananchi ambao ni wakazi wa Mbinga na maeneo mengine hapa Nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI