Header Ads Widget

AJALI YAUA MKOANI NJOMBE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe  Hamis Issa Amethibitisha kutokea kwa vifo vya Watu Nane wa Chama Cha kitume Cha umoja wa Vijana Wakatholiki Njombe (UVIKANJO) waliopata ajali ya Gari aina ya Coaster Iliyogongana na Lori huko Igima Wakati wakitokea Ibumila kuwaona watoto Yatima kwenye moja ya kituo Cha kulelea watoto.


Mbele ya vyombo vya Habari Kamanda Issa amesema ajali hiyo iliyosababisha vifo Hivyo na majeruhi 18 imehusisha Gari aina ya Coaster yenye namba za usajili T 187 CCY Mali ya kanisa Katholiki iliyogongana uso kwa uso na Lori aina ya HOWO Mali ya kampuni ya Specialized Houlage lenye namba za usajili T 108 DYD lililokuwa likiendeshwa na Dereva Hamis Hussein Ramadhan mkazi wa Dar es Salaam.


Aidha Kamanda Issa amesema chanzo Cha ajali hiyo Ni baada ya moja ya Gari aina ya Coaster kuigonga coaster nyingine iliyokuwa kwenye Msafara huo na Kisha moja kupoteza mwelekeo na kulivaa Lori Hilo.


Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Njombe Dkt Winfred Kyambile amekiri kupokea miili ya baadhi ya Watu hao na majeruhi ambao wengine wamewapa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa Mbeya na kwamba vifo Hivyo vimetokana na Majeraha makubwa waliyoyapata Pamoja na kuvuja damu nyingi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI