Na Hamida Ramadhan Dodoma
WAZIRI wa Afya Ummy mwalimu amesema hadi ufikia Machi 15 2022 jumla ya watu elfu 33789 wamethibitika kuwa na virusi vya ugonjwa wa UVIKO 19 huku vifo vikiwa ni 803 kwa muda wa kipindi cha miaka miwili tangu kulipuka kwa ugonjwa huo hapa nchini
Ameyasema hayo leo jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kipindi cha miaka miwili.
Waziri Ummy amesema idadi hiyo ni ndogo kwani serikali ilijikita kupima watu ambao ni wagonjwa na wale wote waliokuwa wakisafiri tu na hawakuwa wakipima kila mtu
Pia amesema zaidi ya watu milioni 2 sawa na asilimia 9.17 ya watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamechanjwa chanjo kamili ya ugongwa wa UVIKO 19 huku akisema idadi hiyo ya uchanjai haridhishi na kuwataka wakuu wa mikoa yote kuendelea kuwahamasisha wananchi kuchanja.
"Mikakati ya serikali ilijikita katika kuwatoa hofu wananchi kuhusu mlipuko huo kwa kufunga shule vyuo na taasisi za elimu za juu na utoaji wa elimu kwa jamii ya kujikinga kwa kukataza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima kunawa mikono kutumia vitakasa mikono kuimalisha huduma za ukaguzi kwa wasafiri wa badari viwanja vya ndege," amesema Waziri Ummy
Aidha amesema kwa kipindi cha miaka miwili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 Tiba asili imeonekana imefanya vizuri kwani imefanya kazi kubwa kwa kuwaondoa hofu wananchi na wannchi kuendelea kutumia.dwa za tiba asili.
"Tiba asili ilituokoa kwa kiasi kikubwa kwa kipindi cha miaka miwili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kutuondolea mzigo katika sekta ya afya kwani ni ukweli kwamba sekta ya afya iko tete wagonjwa kibao miundombinu haitoshi watumishi wachache uhaba wa dawa na vifaa tiba hivyo tuna kwenda kuboresha huduma za tiba asili,"amesema Ummy.
0 Comments