Na THABIT MADAI,ZANZIBAR
WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Masoud Makame amemkabidhi Ofisi Waziri Mpya wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Shaibu Hassan Kaduara huku akiwaomba Watendaji kuendeleza Ushirikiano wa Kazi na Waziri huyo.
Ameyasema hayo Mara baada ya Kukabidhi Ofisi ya Wizara ya Maji,Nishati na Madini ambayo amehudumu kwa Takribani Mwaka na Miezi Mitatu, ambapo Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo Maisara Mjini Unguja.
Amesema kuwa, Watendaji hawana budi kuendeleza Mashirikiano kwa Waziri ili kufikia Malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
“Leo rasmi nmekabidhi ofisi ya Kwa Waziri Mpya na kuwaomba Watendaji kuendelea kumpa Mashirkiano kama walivyonipatia Mimi ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo,”alisema.
Alieleza kuwa yupo tayari kufanya nae kazi kwa Wakati wowote ambao atamuhitaji ili kusukuma mbele Malengo ya Serikali.
“Mimi nmemuahidi kuwa nipo tayari kufanya nae Kazi kwa wakati wowote kumshauri pale ambapo atanihitaji ili kusukuma gurudumu hili pale linapohitajika,” alieleza.
Aliongeza kuwa, amemkabidhi Wizara pamoja na Mashirikia yake ZECO, ZAWA,ZURA pamoja na Miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Wizara hiyo.
“Kuna Miradi Mkubwa unatekelezwa wa Dola Milion 92 wa Ujenzi wa Matangi ambao unajumuisha Ujenzio wa Miondombinu ya Maji Safi na Salama ambapo nmemwambia kuwa kuna uwezekano wa kupata Maji safi na Salama kwa Mwezi Juni hadi Septemba tukaanza kupata huduma ya Maji na kukamilika kwa Mradi huo ni mwezi Januari Mwaka 2023,”alifafanua.
Nae Waziri Mpya wa Maji Nishati na Madini Zanzibar,Shaibu Hassan Kaduara aliahidi kufanya kwa Mashirikiano yaliyotukuka na Watendaji katika kuwahudumia Wananchi wa Zanzibar.
“Pale ambapo Mlimpa Waziri aliepita Mashirikiano ya Kazi basi naomba Misipaachie tuendeleze ili Wanachi wetu wa Zanzibar tuendelee kuwahudumia na kufikia Malengo yaliyokusudiwa,”alisema.
Aidha alisisitiza kwa Watendaji wa Wizara hiyo kwenda kusimamia Nidhamu na Uwajibikaji wa kwa Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi na Idara zilizo ndani ya Wizara ya Maji Nishati na Madini Zanzibar.
0 Comments