Header Ads Widget

WATOTO WACHANGA 296 WAFARIKI BAADA YA KUZALIWA LINDI

 


NA HADIJA OMARY


Jumla ya Watoto wachanga 296  waliozaliwa Mkoani Lindi  kwa kipindi cha Mwaka mmoja uliopita 2021 wamefariki Dunia kwa kukosa hewa .


Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi Rehema Madenge   wakati wa ghafla fupi ya kupokea vifaa tiba kutoka taasisi ya Doris MOllel Fundationi iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi Sokoine.


Bi madenge alieleza kuwa swala la vifo kwa akina mama na Watoto wakati wa kijifungua bado ni changamoto katika Mkoa huo inayohitaji ufumbuzi  kwani kwa mwaka 2021 kati ya akina mama 31109 waliojifungua  watoto 30813 kati yao  walizaliwa wakiwa hai huku Watoto 296 wakipoteza Maisha.


Alisema kuwa sababu kubwa iliyochangia Watoto hao kupoteza Maisha ni kukosa hewa kutokana na Watoto hao kuzaliwa kabla ya wakati ( Njiti).


Hata hivyo alieleza kuwa  Mkoa huo kwa  sasa  una vituo 271  vya kutole huduma za Afya  ambapo kati ya hivyo vituo 254 vinatoa huduma ya Mama Baba na Mtoto huku vituo 17 vikitoa huduma zingine za kawaida.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundationi, BI Doris Mollel  akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo  alieleza kuwa  mashine hizo  9 za kufua hewa ya oxgeni zenye thamani ya milioni 35 zitagaiwa katika Halmashauri tau za Mkoa huo ambazo ni Mtama, Ruangwa pamoja na Mchinga huku akieleza  wanufaika wa mashine hizo ni Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hasa wale wanaopata changamoto ya upumuaji.


Kwa upande wake muuguzi kiongozi wodi ya Watoto wachanga  Clementia Mlope katika hospitali hiyo ya sokoine amesema kwa mwezi wamekuwa wakipokea Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) kati ya 20 hadi 25 kutoka vituo mbali mbali vya kutolea huduma ya afya ndani ya Mkoa ambapo ameeleza kuwa kupewa kwa vifaa tiba hivyo vinaenda kusaidia kwa kiasi kikubwa.



‘’Tunajua hawa Watoto wanazaliwa kabla ya siku zao kwa hivyo hata mapafu yao  yanakuwa hayajakomaa hivyo wanahitaji msaada mkubwa sana wa kupumua kupitia hizi mashine kwahiyo kupatiwa kwa hizi mashine kutasaidia sanakuokoa Maisha ya hawa watoto’’.


Fatuma selemani ni mmoja kati ya akina mama waliojifungua kabla ya wakati aliupongeza uongozi wa Doris Mollel kwa kutoa vifaa hivyo vitakavyoweza kunusuru Maisha ya Watoto Njiti watakaozaliwa hospitalini hapo


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI