Wanufaika wa mradi wa YAM |
Ikiwa katika juhudi za kuwainua kiuchumi vijana na watu wenye mahitaji maalumu serikali kwa kushirikiana na wadau kutoka mradi Youth Agency Mufindi (YAM)wameandaa mafunzo kwa vijana mbalimbali ili kuwasaidia kufikisha ndoto zao.
Wakizungumzia kuhusu malengo yao baada ya kufika kwenye mafunzo hayo wanufaika hao wamesema wamejipanga vyema katika kuyapokea mafunzo kwani wanaamini ndoto zao za muda mrefu zitatimia lakini pia wataweza kumudu maisha yao pamoja na kuzikabili changamoto za maisha kwa ujumla.
Mwezeshaji wa mafunzo |
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Heriel Mfangavo amesema mafunzo hayo yamejikita katika kuwasaidia vijana namna ya kujitegemea katika nyanja zote ili waweze kujikwamua katika changamoto wanazozipitia lakini pia kujiinua kiuchumi kwa kufanya shuguli mbalimbali za ujasiriamali
Dkt Mfangavo ameongeza kuwa vijana ambao wanastahili kukaa kwenye makundi baada ya mafunzo hayo wananufaika kwa kupata mikopo kutoka katika bajeti za halmashauri ambayo itawasaidia katika kuendeleza biashara zao lakini pia vijana ambao ni walemavu wanapewa kipaumbele cha kuweza kukopeshwa au kuingizwa kwenye fursa za ajira rasmi .
Meneja wa mradi YAM |
Meneja wa mradi wa YAM Zilpa Mgeni wakati akitolea ufafanuzi kuhusu ushirikiano wa mradi na serikali amesema wanaishukuru serikali kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na mradi wao ambao kiujumla una msaada mkubwa sana kwa vijana
''Mimi na timu yangu tumeona huu mradi unasaidia kwasababu tumegundua kuwa kuna mbadaliko makubwa tangu tumeanza kuwabainikwani hapo mwanzo walikuwa hawajiaamini kwamba wanaweza kufanya biasharalakini baada ya kupata mafunzo ya saikolojia na ujasiriamali wao wenyewe wamekiri kwamba wanaweza kufanya kitu ''. Amesema Zilpa
Pia ameongeza kwa kuiomba serikali kuzidi kutoa ushirikiano hasa kwa kusaidia kupatikana kwa mikopo hiyo ili wanufaika hao wapate mitaji na kuweza kujiendeleza kimaendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi na diwani wa kata ya Luhunga Festo Elia Mgina amewataka vijana hao kusikiliza vyema mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwa pamoja na kuwahakikishia kupata mikopo baada ya mafunzo yao kutokana na serikali kujipanga vyema katika kuwasaidia wahitaji. |
Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule wakati akifungua mafunzo hayo amewataka vijana hao kuzingatia masomo yao na kutokukatishwa tamaa na changamoto wanazokumbana nazo bali wajipe moyo na kuamini kuwa wakati wao wa kuinuka ni sasa hivyo hawana budi kukabiliana na changamoto hizo.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi |
Aidha amewasisitiza kutumia fursa hiyo ya mafunzo vizuri kwani serikali ya awamu ya sita ya rais samia suluhu hasan imejipanga vyema kuwainua na kuwasaidia wahitaji wote kutokana na kutenga fedha nyingi katika halmashauri zao hivyo wanachotakiwa kufanya ni kujitambua .
Pia ameongeza kuwa baada ya kupata mafunzo hayo jambo la msingi ni kuyatekeleza kwani utekelezaji wao utapunguza mazingira ya vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia katika jamii zao huku akiwataka kuwatumia viongozi wao wakati wanapohitaji msaada .
0 Comments