Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUSAIDIANA NA SERIKALI KATIKA KIPINDI CHA MWEZI MTUKUFU

 



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wafanyabiashara Nchini kuisaidia Serikali katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuhakikisha Chakula kinapatikana cha kutosha.


Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ameyaeleza hayo leo wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Wafanyabiashara Ofisini Kwake Vuga Mjini Unguja ambapo amefahamisha kuwa, Jukumu la Serikali ni kuhakikisha Chakula kinakuwepo kipindi chote na kueleza kuwa SMZ inafarijika kuona Wafanyabiashara hao wanaisaidia Serikali katika upatikanaji wa Chakula Nchini.


Amesema  kuwa hadi sasa hakuna viashiria vyovyote vya upungufu wa Chakula Nchini hatua ambayo Serikali  inamatumaini makubwa kwa wananchi wake kupata huduma hiyo bila ya changamoto yoyote.


Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka Wafanyabiashara hao kuhakikisha wanauza Biashara kwa kufuata bei elekezi na kukemea tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara ambao hupandisha bei katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Mhe Hemed amesema Wafanyabiashara hao ni vyema kusimamia makubaliano na Taasisi husika juu ya bei za Bidhaa ili kutomsumbua mwananchi anaetafuta huduma muhimu za vyakula. 


Akizungumza kwa niaba ya Wafanyabiashara wenzake  Said Nassir Nassor Bopar ameeleza kufurahishwa kwao kwa kitendo cha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwaita na kujadiliana nao kuhusu uwepo wa vyakula katika vipindi vyote hasa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.


Aidha amewashauri Wafanyabiashara wenzake kutopandisha biashara kiholela hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa nia ya kupata faida kubwa zaidi na kuwasihi kuendelea kufanya biashara zao kwa mujibu wa makubaliano na Serikali



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI