Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHAMASISHA ZOEZI LA SENSA

 




Teddy Kilanga.



Arusha.Spika wa bunge Mstaafu na Kamisaa wa sensa,Anna Makinda amewahakikishia viongozi wa dini na wakimila  kuwa zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika Agasti mwaka huu litakuwa shirikishi ili kuweza kupata taarifa sahihi zitakazokwenda kutumika na serikali katika mipango yake ya sasa na baadaye.



Aidha amewataka viongozi hao kuhamasisha jamii katika kutoa elimu  juu ya zoezi hilo ili kupata taarifa sahihi za dodoso la sensa 



Akizungumza katika semina ilishirikisha vijana,viongozi wa dini mbalimbali na Maleigwani iliyofanyikia jijini Arusha,Makinda amesema zoezi hilo la sensa litaisaidia serikali kuweza kuwahudumia makundi yote ikiwemo wafugaji  katika kuwatafutia maeneo.



"Huduma zote zitapatikana endapo zoezi la sensa litafanyika kwa usahihi na kuisaidia serikali kufahamu maeneo yanayohitajika na wafugaji kwa ajili malisho hata wakulima,"amesema Makinda.



"Ili serikali ijipange vizuri katika kutoa huduma mbalimbali lazima idadi ya watu ijulikane kupitia sensa hii na itakuwa shirikishi kwa lengo la kupata taarifa kutoka kwa wananchi waliopo kwenye maeneo husika ambapo dodoso lake litauliza maswali wahusika kwa kila eneo,"amesema Kamisaa wa Sensa Anna Makinda.



Aidha Kamisaa huyo amesema kupitia sensa hiyo serikali itafahamu changamoto za kila maeneo na kuyafanyia ufumbuzi kwa wakati kupitia zoezi hilo la sensa watapata majawabu ya changamoto za wananchi.



Kwa upande wake Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya takwimu ,Mdoka Omary amesema sensa ya mwaka huu ni jumuishi ambayo inahusisha majengo na anuani za makazi ambapo watachukua taarifa zote ikiwemo umri,jinsi pamoja na hali ya ulemavu nchini.



Omary amesema pia watachukua taarifa za uamiaji,elimu,vifo na vyanzo vyake pamoja na hali ya makazi na dodoso la sensa litasaidia serikali katika mipango yake mbalimbali ya kimaendeleo.



"Kwenye sekta ya afya ,elimu pamoja na nyingineza wanategemea sana takwimu katika mipango ya maendeleo na zoezi hili ni shirikishi hivyo wahusika tunaowategemea ni jamii na tunachosisitiza ni kupata taarifa sahihi,"amesema Mtakwimu huyo.



Naye Leigwanani Mkuu jamii ya wamasai ,Isack Eliksongo ameahaidi ushirikiano katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa zoezi ili huku akiwasisitiza vijana kuwa wazalendo katika kulisaidia Taifa lao kufanikisha zoezi hilo.



Baadhi ya viongozi wa dini wamesema wako tayari kuisaidia serikali kufanikisha zoezi hilo kwani litasaidia kutatua changamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo migogoro ya ardhi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI