Na Mwandishi wetu, Mtwara
Mmlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na kiwanda cha Saruji Dangote wameingia makubaliano ya kibishara kwaajili ya kutumia bandari hiyo kusafirishia shehena ya saruji.
Makubaliano hayo yamekuja baada ya bandari hiyo kuongezewa uwezo wa kusafirisha shehena nyingi zaidi na serikali ya awamu ya sita ambayo ni matokeo ya utelekezaji wa mwaka mmoja wa Rais Samiah Suluhu katika uboreshaji wa bandari nchini.
Akiingia makubaliano hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TPA Lyidia Malya alisema wana mikakkati ya kuwezesha bandari ya Tanga, Dar na mtwara kufanya kazi kubwa ili kuongeza ajira nchini.
alisema kuwa uboreshaji wa huduma hizo unaenda sambamba na fursa mbalimbali ambapo makubaliano hayo yatongezea wigo wa utendaji kazi wa bandari hizo.
Tunapoboresha huduma za bandari tunaamini kuwa hata fursa nyingi zitafunguka sio kwetu hata kwa wananchi wa mikoa huisika ndio naamini makubaliano haya ni chachu ya kufanya makubwa zaidi katika kuboresha uchumi wa mwananchi na nchi kwa ujumla”
Kwakutumia usafiri wa maji tunaokoa miundombinu yetu ya barabara ambayo imekuwa ikiharibika kwakutumiwa na magari makubwa ambayo yanayosafirisha bidhaa mbalimbali kutoka mikoa husika” alisema Malya
Kaimu Meneja wa TPA Mtwara Norbert Kalembwe alisema awali kiwanda hicho kilikuwa kikitumia barabara kufsafirisha saruji hivyo kusabnabisha uharibifu wa miundombinu.
Ambapo upanuzi wa huduma kwa sasa saruji inatajia kusafirishwa kwenda nchini madagaskar ambapo awali ilikuwa ikifika msumbiji kaskazinii pamoja na chini Comoro.
Nae Meneja wa Kiwanda cha Saruji Dangote Nchini Tanzania Abdullahi Baba amefurahishwa na makubaliano hayo ambayo kwake ameona kama ni hatua kubwa kibiashara hivyo kupunguza umbali mrefu waliokuwa wakisafisha bidhaa hizo kwenda maeneo mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi hivyo ushindani kuwa mgumu sokoni.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti alisema bandari hiyo imeweza kusafirisha makaa yam awe kwenda nchini india kwa zaiid ya tani 30-50 kwa mwezi na pia imweza kusafirisha mafuta tani milioni 6 kwa mwaka.
“ Kwasasa Bandari ina uwezo mkubwa na tunaamini kuwa itaweza kufanyakazi kubwa zaidi kadri itakavyopewa hivyo kitendo cha kufungua fursa kina tija kubwa kwa mkoa na taifa kwa ujumla
“uwekezaji huu wa upanuzi wa bandari utawezesha wawezekezaji kufurahia mazingira ya uwekezaji nchini hali ambayo itatupa mwanya wa kuongeza bidii na kuzitafuta fursa kwa mataifa mbalibali duniani.
0 Comments