Na Hamida Ramadhan Dodoma
MRADI wa ujenzi wa soko la wafanyabiashara ndogondogo (Machinga Complex) Jijini Dodoma umesaidia kuokoa gharama za watumishi wa serikali wakiwemo,wakurugenzi,wakuu wa wilaya,makatibu tawala,na wakuu wa wilaya kwenda nje ya nchi kujifunza kujifunza utekelezaji wa miradi inayofanana na huo.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Serikali za mitaa na Tawala za Mikoa [TAMISEMI] Innocent Bashungwa wakati akizungumza kwenye mradi wa ujenzi wa Machinga Complex baada ya baadhi ya wakuu wa mikoa hapa nchini kutembelea mradi huo kwa ajili ya kujifunza.
Aidha,Waziri Bashungwa amesema baada ya baadhi ya wakuu hao wa mikoa pamoja na makatibu tawala kujifunza utekelezaji wa mradi huo itawasaidia kufanya miradi yenye ubora inayofanana na mazingira wanayotoka .
"Niwatake wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kuwa wabunifu katika utekelezaji wa miradi inayokwendana mazingira halisi ya watumiaji," amesema Bashungwa
Nao baadhi ya wakuu wa mikoa waliofika katika soko la Machinga Complex wamesema watahakikisha wanajenga masoko ya viwango katika maeneo yao baada ya kujifunza muonekano wa soko hilo.
Mkurugenzi wa kampuni ya MOHAMMED BUILDERS inayotekeleza mradi wa soko hilo,TAHER JAFFERTI ameupongeza mkoa wa Dodoma kwa kuwa imara katika usimamizi wa utekelezaji wa mradi huo huku mshauri mwelekezi wa mradi huo Dkt.Ibrahim Msuya akibainisha vigezo muhimu wa utekelezaji wa mradi wa soko hilo.
Miongoni mwa Wakuu wa mikoa waliotembelea kujifunza katika soko la Machinga Compex Dodoma ni kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Songwe, Morogoro, Iringa na Mwanza ambapo kati ya Tsh.Bilioni 5 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu ya Machinga,Milioni 500 imeletwa utekelezaji wa soko la Machinga Complex huku ujenzi ukitarajiwa kukamilika mwezi Mei Mwaka huu.
Mwisho.
0 Comments