Mwandishi Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka amesema Halmashauri Kuu ya CCM Tiafa imemteua Abdurahman Kinana aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho kushika nafasi ya umakamu Mwenyekiti Bara wa CCM Taifa baada ya Philip Mangula aliyedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kung’atuka.
Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia Mkutano Mkuu Maalaum unaotarajiwa kufanyika jijini Dodoma kesho amesema kiongozi huyo amefikia uamuzi huo ili kukidhi ya matakwa ya katiba ya chama hicho.
Amesema Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea rasmi ya kung’atuka kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula ambaye amefikia uamuzi huo kukidhi matakwa ya katiba ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Baada ya kupokea ombi la Mangula wajumbe wa Halmashauri Kuu wamefanya uteuzi wa Abdurahman Kinana atakayepelekwa kwenye Mkutano Maalum kugombea nafasi hiyo,”amesema
Hata hivyo amesema Halamshauri Kuu imemsamehe aliyekuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne Bernard Membe na Abdallah Maulid Diwani kutokana na makosa wayoyafanya huko nyuma.
Aidha amesema pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea na kupitisha azimio la mkutano Mkuu Maalum ambayo kwa kawaida hufanyika mara tatu katika kipindi cha miaka mitano.
Amesema Mkutano huo unaofanyika leo umekidhi vigezo vyote vya kikatiba na maandalizi yote yamekamilika na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa amekagua na kuridhishwa na maandalizi hayo.
0 Comments