Header Ads Widget

RC MTAKA AUAGIZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA KUUNDA KAMATI YA KUWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA SOKO LA SABASABA KUPISHA UJENZI.

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma 


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya jiji kuunda kamati itakayo shughulikia mchakato wa kuwahamisha wafanyabiashara wa soko la Saba Saba ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa.


Pia amesema wafanyabiashara wa soko hilo ambao ni zaidi ya 7000 wapewe taarifa ya kuhamishwa kabla ya miezi 4 ya kupisha ujenzi huo.


Mtaka ameyasema hayo  jijini hapa katika kikao na wafanyabiashara hao chenye lengo la kujadiliana namna mchakato wa kuhamishwa utakavyofanyika kwa kufuata utaratibu maalumu, amesema katika mchakato huo itaundwa kamati itakayoshirikisha wafanyabiashara hao jiji na ofisi ya wilaya lengo likiwa ni kuondoa migongano  baina ya wafanyabishara serikali ya mkoa huo.


Amesema kabla ya mchakato wa kuhamishwa wafanyabiashara hao utafanyika upya usajili na kwamba atakayekutwa kwenye sehemu yake ya biashara ndiye atakayesajiliwa.


"Najua kuna watu hawapendi huu mchakato ni kwa kuwa wanamiliki vibanda vingi ambavyo wamevipangisha na wanapokea kodi," amesema Mtaka.


Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kamati hiyo itajadiliana katika vikao vyao vya ndani na kupendekeza sehemu tatu ambazo wafabiashara hao wataenda kukaa kwa muda ili kupisha ujenzi wa soko hilo.


Ameongeza kwamba baada ya kupendekeza maaeneo hayo kamati hiyo itarudi kujadiliana na wafanyabiashara hao.


Amesema kuwa jiji la Dodoma linakua kwa kasi kubwa katika maendeleo ili kuendana na kasi hiyo ni vema wafanyabiashara wakafanya biashara zao katika mazingira  yenye hadhi ya jiji hilo.


Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma mjini  Anthony Mavunde amewaomba wafanyabiashara hao kutokuwa wabishi kupisha ujenzi huo muda utakapofika.


" Kila mfanyabiashara atapata haki yake niwaondoe wasi wasi kutawa na utaratibu mzuri wa kuhamishwa katika eneo hili," amesema Mavunde.


Ameeleza kuwa  kila mfanyabiashara  atapata nafasi,kiizimba cha kufanyia biashara  kwa muda na baada ya ujenzi wa soko hilo la sabasaba kukamilika kila mtu atarudi katika nafasi yake .


Akiongea kwa niaba ya wafanyabishara wenzake mfanyabishara Stephane  Massawe amesema wao kama wafanyabishara hawajagoma kuondoa lakini wanaomba taarifa kuwa ni lini wanaondo katika soko hilo kupisha ujenzi huo.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI