Header Ads Widget

MABINTI WALIOPATA MIMBA ZA UTOTONI WASHUKURU MRADI WA YAM KUWAFIKIA

 

MABIBTI waliopo kwenye Mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) ambao walikatisha ndoto za maisha baada ya kupata mimba za utotoni wameshukuru mradi huo kuwafikia na kuahidi kuja kuwa na mafanikio ya kiuchumi .

Wakizungumza na Matukio DaimaTv wakati wa mafunzo ya siku 10 yanayoendelea Ukumbi wa Yatima Igoda wilaya ya Mufindi Anles Msindila ,Debora Mdobofu na Adelina Hawa wamesema mbali ya ndoto zao kukatishwa na mimba Kwa Sasa wanajitambua na wamejipanga kuwa wajasiriamali Wazuri baada ya mafunzo hayo .

Pia mabinti hao wametoa Rai Kwa wenzao waliopo mashuleni kuzingatia masomo na kuachana na  haraka ya maisha Kwa kupenda tabia za mahusiano ya kimapenzi  wakiwa wadogo 


Mradi wa YAM unatekelezwa kwenye vijiji 16 na kata tatu za Luhunga ,Mdabulo na Ihanu  unaendeshwa Kwa ushirikiano  na serikali  ya Halmashauri ya Mufindi  mradi ambao kiujumla una msaada mkubwa  kwa vijana  na ni miaka minne toka mwaka 2021/2024 umefadhiliwa na    serikali  ya Finland  chini ya taasisi yake ya Diaconess   kwa  ushirikiano  wa  serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi na taasisi ya  Foxes Community and Wild Life Conservation.(FCWC)


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI