Header Ads Widget

KAYA TAKRIBANI 600 ZAILILIA SERIKALI


Na Hamida Ramadhani,MDTV Dodoma

ZAIDI ya Kaya takribani600  zilizokuwa zikiishi eneo la chanzo Cha Maji Mzakwe katika Kata za,Mndemu,Gawaye,Mchemwa,Chihanga,Makutupora,pamoja na Mndemu wameiomba Serikali kuwalipa fidia kwani ni muda mrefu tangu waondolewe kupisha eneo hilo na hivyo kusababisha kuwepo mgogoro katika eneo la chanzo hicho ikiwemo kutostawi kwa miti ya eneo hilo inayotakana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na shughuli za kibinadamu hasa kuingiza mifugo.


Hali hiyo imejitokeza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kutembelea katika chanzo cha maji Mzakwe kujionea  hali halisi ya mgogoro na kusikiliza kero za wananchi  katika eneo hilo ambalo serikali imeweka mkakati  kabambe wa upandaji miti.



Akiongea  kwa niaba ya wananchi wenzake mbele ya Mkuu huyo wa mkoa Mzee Shabani Nyambo amesema wananchi wote waliokuwepo wakiishi katika maeneo hayo wanamanu'guniko kutokana na kuondolewa katika eneo hilo liliotengwa kwaajili ya msitu bila kulipwa fidia huku wengine wakilia kulipwa fidia ndogo na serikalli.


"Sisi wananchi hatukuibishia serikalli tulupoambiwa tunatakiwa kupisha eneo hilo tulikubali kuondoka lakini cha kushangaza wakati wa malipo watu tililipwa pesa ndogo hadi aibu kusema mbele ya hadhara hii," amesema  Mzee Nyambo.


Na kuongeza "Hapa bila ya kuelewana hakuna kitu kitakacho fanywa na kuonekana Mimi nawahakikishieni kuwa tukikaa pamoja na kuelewana mkatulipa fidiaHapa miti hii inayogoma kuota nasema miti itapandwa na kukua,"amesema na kusisitiza Mzee huyo


Kufuatiana kuwepo kwa malalamiko hayo,Mtaka  ameziagiza Taasisi zote zinazohusika na uratibu bonde la maji katika chanzo cha maji Mzakwe mkoani Dodoma kukutana  ofisini kwake siku  ya jumatatu pamoja na wajumbe Zaidi ya 15 ili kuleta suluhu ya mgogoro huo ambao ni wa muda mrefu huku akiagiza Taasisi hizo kuja na Mpango kabambe wa kuanzisha uratibu wa maandalizi ya upandaji wa miti katika ekari 309  za mfano katika chanzo hicho cha maji.

  

Sanjari na hilo,Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amezitaka Taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo,jiji,pamoja na Mamlaka ya Bonde hilo kufanya maandalizi huku akisema utatuzi wa mgogoro na wananchi ni siku ya Jumatatu ambapo mkutano huo utahusisha wajumbe 15 kutoka maeneo yenye mgogoro.


"Tunaanza maandalizi ya kupanda miti kwenye msimu wa mwaja 2022 hadi 2023 eneo hilo la Mzakwe eneo lenye ukubwa la ekari 309 hivyo viongozi Wote na wataalamu wote wa misitu na udogo mshilikiane kuhakikisha eneo la chanzo cha maji Mzakwe panakuwa msitu,"amesema Mtaka.


Baadhi ya viongozi ikiwemo kikosi cha kustawisha eneo la chanzo cha Maji Mzakwe wamesema watahakikisha wanatekeleza maagizo hayo katika kuhakikisha eneo hilo linakuwa la kijani .


Naye ProfesaSalim  Maliondo kutoka chuo cha Sokoine (SUA) amesema wanapokea maelekezo hayo na watashirikiana na Mkuu huyo wa bonde kwaajili ya kuanza kazi ya upandaji miti katika eneo hilo







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI