Header Ads Widget

"HAMASISHENI WANANCHI KUANZISHA UFUGAJI MAZAO YA BAHARI"_ULEGA



HADIJA OMARY _Lindi


Naibu waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amewataka viongozi katika ngazi za halmashauri zilizopo pembezoni mwa ukanda wa bahari ya hindi kuwahamasisha wananchi kuchangamkia fursa ya ufugaji wa mazao ya Bahari katika maeneo yao.


Ulega ametoa agizo hilo alipokuwa anazungumza na viomgozi hao kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara katika kikao kazi kilichofanyika Mkoani Lindi chenye lengo la kutambulisha, kuhamasisha, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kutumia rasilimali za mazao ya bahari kibiashara.


Ulega alisema kuwa  licha ya kwamba Tanzania imebahatika kuwa na rasilimali nyingi hasa  zinazohusiana na uvuvi pamoja na fukwe zilizosheheni rasilimali  ambazo ni fulsa kwa wananchi wanaoishi kanda hizo  kuweza kuwekeza na kujiongezea kipato lakini bado fukwe hizo azijatumika kikamilifu .


"ili fukwe hizo ziweze kutumika kwa tija ni wajibu wetu sisi kama viongozi kuwa na dhamira ya dhati ya kuwasaidia wananchi hawa kwa  kuwahamasisha  ili   kuzitambua fursa zilizopo na baadae kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Nchi kwa ujumla"


Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Mkuu wa Wilaya hiyo , Shaibu Ndemanga alisema  licha ya kipato kidogo kinachopatikana kutokanana na Samaki kwa sababu ya uvuvi kuwa duni Mkoa huo umejipanga kuhakikisha unaboresha sekta hiyo ya Uvuvi.


Alisema  katika kuhakikisha Eneo la ufugaji wa samaki Elimu inatolewa kwa kiwango cha juu Mikoa hiyo miwili ya Lindi na Mtwara tayari imeanzisha shamba Darasa katika Halmashauri ya Mtama litakalotumika kuzalishia mbegu za samaki pamoja na  Darasa kwa wafugaji hao


Nae Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Kilwa  Ally Kasinge alisema kuwa Mpango huo ulioletwa na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaonyesha ni kiasi gani serikali imeamua kuwashika Mkono wavuvi.


"Huko nyuma sekta hii ya uvuvi ni kama vile  wavuvi walikuwa wameachwa wenyewe pasipo kuwa na msaada wenye kuonekana kutoka  Serikalini , mathalani sisi wavuvi wa Wilaya ya Kilwa tulikuwa tunatumia fursa ya bahari katika utaratibu wa kawaida lakini kwa mpango huu ambao Wizara imekuja nao ni wazi kuwa Wananchi wanakwenda kuelimishwa namna bora ya uvuvi pamoja na ufugaji wa mazao mengine ya bahari"  alifafanua Mh. Kasinge



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI