Na Titus Mwombeki-MTDTV BUKOBA.
Chama kikuu cha ushirika mkoani kagera (KCU 1990 LMD) kinachojihusisha na kukusanya kahawa wa kahawa kutoka kwenye vyama vya msingi ambavyo ni wanachma wa KCU katika baadhi ya wilaya mkoani kagera kimetoa zaidi ya shilingi bilioni moja kama nyongeza ya makipo ya zao hilo.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Ressy Mashulano wakati akizunguza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi ya chama hicho ulioko Manispaa ya Bukoba mkoani kagera ambapo amesema kuwa kama yalivyo majukumu ya chama hicho kuhakikisha wakulima wa zao la kagawa mkoani Kagera wananufai zaidi, chama hicho kimetoa fedha hizo kama nyongeza ya malipo ya zao hilo kwa msimu wa 2021/2022.
“ Wakati tunaelekea kwenye msimu mwingine, chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera kimeweza kutoa kiasi cha fedha bilioni 1.4 na hii nikutokana na kile tunachokipata ndo hicho tunakirudisha kwa wananchi ambao ni wakulima, kwahiyo wananchi kwa msimu huu tumeweza kuwarudishia shilingi bilioni 1.4 na ongezeko hili ni matokeo na matunda ya ushirika ambao moja ya majukumu yake ya msingi ni kutafuta masoko bora ya kahawa kwa manufaa ya wakulima”
Kwaupande wake makamu mwenyekiti wa chama hicho Respicus John amesema kuwa, chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU 1990 LTD) kupitia kwa viongozi wa chama hicho wamepanga mikakati mbalimbali ili kuhakikisha chama hicho kinakata kiu ya wakulima wa zao la kahawa mkoani Kagera.
“Tumepanga mpango mkakati kwa miaka mitano (5) ambao umesheheni mambo mbalimbali,tuna mradi mkakati ambayo tumejipanga kuifanya kama vile mradi wa kilimo cha kahawa katika mashamba yetu ya chama ambayo yatatumika kama shamba darasa hapa mkoani kagera, kuanzisha ujenzi wa miradi ya vitega uchumi kwani mnajua kuwa chama chetu kimewekeza katika majengo na tunayo aridhi tupu inayoitaji kuendelezwa pamoja na majengo ambayo hayajafikia kiwango kwahiyo kupitia wadau mbalimbali tutahakikisha tunayaendeleza na tunaamini kuwa endapo miradi hii ikitekelezwa itaweza kubadili sura ya mji wetu wa Bukoba na kuongeza mapato ya ndani ya chama ili chama chetu kiweze kujiendesha chenyewe tutokana na miladi hiyo”.
Ameongeza kuwa, chama hicho kimejipanga kuanzisha mfuko maalumu ambao utawawezesha wakulima wa kahawa kuweza kukopeshwa fedha ili kuweza kukidhi mahitaji yao kwani wakulima wengi vijijini wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kukoswa mikopo suala ambalo limepelekea wananchi hao kipindi amchacho sio cha msimu kuuza kahawa zao kwa njia za ‘obutula’ .
“Kupitia mfuko huu maalumu kama mambo yataenda vizuri wakulima watakuwa wanakopa fedha kipindi ambacho sio cha msimu na wakati wa msimu unapofika basi wanaleta mazao yao kwaajiri ya kulipa mkopo huo “ amesema John.
Sambamba na hayo, chamo hicho kimedhamilia kuanzisha ‘coffee bar’ nzuri na ya kisasa ambayo wageni kutoka nje pampoja na mkoa wa Kagera watatumia kujipatia kinywaji cha kahawa kwani kupitia hii itakuwa kichocheo kwa watu wengi kutoka nje kunua kahawa inayozalishwa mkoni humu.
0 Comments